HATIMAYE WANARIADHA WAWILI WAONDOKA ALFAJIRI YA LEO; WAAMBWA WAENDE NA BUKTA NA SINGLET ZA LINING, KAMA HAWANA WAAZIME UDHAMINI WAO UMEKWAMA

 


 Baada ya viongozi wa RT kutangulia Moscow wiki jana hatimaye
wanariadha wawili wameondoka leo kwa kutumia shirika la ndege ya
Uturuki (Tarkish Airlines) kwenda Moscow Urusi. Wanariadha hao
wanaokusudiwa kushiriki mbio za Marathon ni Msenduki Mohamed na
Phaustin Musa ambao pia walikuwemo katika timu iliyokwenda Olimpiki ya
London mwaka jana.
 
Kabla ya kuondoka mmoja wao alihangaika usiku na mchana kutafuta namna
ya kupata kibali cha kikazi (JWTZ), jukumu ambalo lingetakiwa
kusimamiwa na viongozi wa RT waliotangulia ama basi wale waliobakia
ofisini. Hata hivyo siku nne zilizopita (mimi) niliongea na
mwanariadha huyo ambaye alionyesha hali ya kukata tamaa kwa kile
alichodai kwamba "kazi yangu ni kufanya mazoezi ili nikaiwakilishe
nchi yangu kwa uwezo wangu wote, hata hivyo kwa sababu wahusika wa RT
hawanipi ushirikiano itabidi nijitose kwani Tanzania ni nchi yangu
pia", alisema mwanariadha huyo ambaye aliomba namba ya simu ya ofisa
moja mstaafu wa jeshi amjulishe hali halisi. Kwa bahati
nzuri namba nilikuwa nayo nikampa.
 
Kalenda ya IAAF: Ni lazima kila taifa liwe limekamilisha mashindano
yake kabla ya mashindano yoyote makubwa ya ngazi za dunia, ikiwemo
Olimpiki, Mashindano ya dunia na Jumuia za madola, ili kwamba
wanariadha watakaofanya vizuri katika mashindano ya mataifa yao waweze
kuchaguliwa na hatimaye kuwakilisha nchi zao. Huo ndio utaratibu
unaopaswa kufuatwa na nchi zote zilizopo chini ya uanachama wa chama
cha riadha cha dunia (IAAF). Tanzania eti tunatarajia kufanya
mashindano ya taifa mwishoni mwa Agosti!, kwa maana nyingine watanzania
wajiulize; Je watakaofanya vizuri hapo watakwenda wapi?, au basi
wataambia asanteni sana, tunawapenda sana ila tafadhali rudini
makwenu?. 'Utawezaje kurukia mtihani wa kidato cha nne alafu bado uwe
na haja ama sababu ya kulazimika kufanya mtihani wa darasa la saba'!.
 
RT wameamua kuvunja sheria zote: Watanzania tushirikiane kwa hili kwa
kufanya utafiti kabla ya kufanya maamuzi, sababu IAAF ni
taasisi inayofanya kazi zake kwa uwazi na kila mtu anaweza kupata
habari zote wakati wowote. IAAF inaipatia RT fedha kila mwaka kutokana
na maendeleo ya riadha (performance), Tanzania imekuwa ikipata kiwango
cha chini kabisa kila mwaka kwa sababu performance yake ni mbovu, (USD
15,000) sawa na TSH: 24,750,000/ kwa mwaka.Jiulize ni lini watanzania
tumeshawahi kupewa 'mapato na matumizi' ya fedha hizo, pia jiulize
ni kwa vipi wameshindwa hata kuimarisha ofisi yao ili hata
watanzania wawe na imani na hata kufungua mioyo na pochi zao ofisini
hapo?. Je wajua kwamba kila mara dola hizo zinapoingia RT wanakimbilia
kuitisha kikao cha kamati ya utendaji Morogoro ili wapange mgawanyo wao?. KAMA
HIVYO SIVYO BASI WASEME FEDHA ZA IAAF ZINAFANYA KAZI GANI.
 
LINING: Ni kampuni ya kichina ambayo kwa kweli iliwahi kudhamini
mchezo wa riadha hadi pale ambap vigogo wawili walipon'ga'ngania
mikate yao wakiwa Beijing China 2008 katika mashindano ya Olimpiki,
ambapo bosi wa TOC alitumia ubabe ili PUMA itumike wakati bosi wa RT
wa wakati ule naye akitaka LINING itumike maana kila mmoja wao
aliahidiwa 'bahasha la pembeni' iwapo Tanzania itatumia vifaa vyao.
Bosi wa TOC alimbwaga bosi wa RT na hivyo PUMA kutumika Beijing. Hata
hivyo vita vya wawili hao viliisababishia Tanzania maumivu ya
kuonekana matapeli na hatimaye kampuni zote mbili kuondoa udhamini.
SASA TUNASHANGAA NINI TUKIONA WANRIADHA WETU WANA PIGA KAVU KAVU (PEKU).
 
WANARIADHA: Wanariadha wetu wawili ni wakimbiaji safi sana, ila
tungeweza kuwapata wakimbiaji safi zaidi kungelifanywa mashindano ya
taifa ili kuchagua timu kubwa zaidi katika mashindano yote (Mita 100,
200, 400, 800, 1,500, 5,000, 10,000 na Marathon) kwa wanaume na
wanawake bila kusahau miruko na mirusho (Field Events). Hata hivyo
taifa lisidanganywe na ndimi zilizojaa uongo wa kisiasa; 'HAKUNA
MEDALI MOSCOW' kutokana na uharamia wote huo niliouelezea. "WALIAMBIWA
WAENDE NA VIFAA VYA LINING, KAMA HAWANA WAAZIME", chanzo cha kuaminika
kilisema. Je viongozi hawa wawili waliotangulia wameshindwa vipi
kuandaa hata vifaa vya kukimbilia (gear), hii ni kutokana na 'bridge
of contract' iliyotokea wakati wa PUMA na LINING, 'MATOKEO YATATHIBITISHA UKWELI'.

Comments

  1. it was painful to watch other athlets from other country win medals... keep exposing these idiots!!!

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga