Latest News

Friday, March 14, 2014

Suleiman Nyambui: Tujitoe katika mashindano ya Jumuia za Madola

Suleiman Nyambui
Akizungumza na shirika la habari la BBC leo asubuhi Suleiman Nyambui alikiri Tanzania haina uwezo wa kupata medali hivyo ni bora tukajitoa kukwepa aibu.

Nyambui amekaririwa akisema hivyo wakati siku chache zilizopia alikaririwa na Star Tv akijigamba kwamba sasa tutashinda medali baada ya kuwepo na taarifa kwamba timu za Tanzania zitapelekwa nchi za nje kufanya mazoezi kwa msaada wa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe.


Tuamini lipi kati ya maneno yaliyosemwa na mtu huyo huyo katika vyombo tofauti vya habari?

No comments:

Post a Comment