RIADHA: Tunawatakia maandalizi na ushiriki mwema Ngorongoro Half Marathon


Kesho April 19, 2014 wilayani Karatu mamia ya wanariadha watashiriki mashindano yenye kubeba jina maarufu sana Africa na ulimwenguni kote, jina ambalo linatokana na ‘Ngorongoro Crater’

Sisi waandaaji wa Sokoine Mini Marathon tutajifunza mengi kutoka kwa wenzetu wa Ngorongoro Half Marathon kwani wao ni wakongwe katika maandalizi ya mbio kubwa hapa nchini.

Pia tunawapongeza wanariadha waliojitoa kushiriki mbio mbili ndani ya wiki moja, bila shaka ni kwa ajili ya uzalendo wao na mapenzi yao kwa mchezo wa riadha.

Tunaamini kwamba hivi sasa Tanzania ipo katika ‘mpito’ wa kutafuta namna bora ya kurudisha heshima katika riadha; Heshima iliyoletwa hapo zamani na akina John Steven Akhwari, Filbert Bayi, Gidamis Shahanga, Juma Ikangaa, Mwinga Mwanjala, Suleimana Nyambui nk.

‘Tunawatakia Ijumaa Kuu njema, mashindanomema na hatimaye Pasaka njema’

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga