Latest News

Tuesday, April 15, 2014

SOKOINE DAY RUN: Shukurani na pongezi kwa watanzania wote


Ilikuwa siku ngumu yenye changamoto nyingi iliyosababishwa na hali ya mvua, lakini ilikuwa ‘Mission Accomplished’ Asante mheshimiwa rais na Spika wa bunge kwa kuja kutuunga mkono.
Kwa kumbukumbu zangu sijawahi kuona msafara mkubwa wa kitaifa ulioongozana na msafara wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ilikuwa fursa nzuri ya kuwaona watawala wa nchi hii inayoelekea kuadhimisha NUSU KARNE ya muungano wake uliojaa historia ya pekee na amani. 
 Msafara huo uliwajumuisha watu maarufu ambao ni pamoja na rais mstaafu Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wastaafu Salim Ahmed Salim na Edward Lowassa, Mama Maria Nyerere, Spika wa Bunge Anna Makinda, waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenela Mukangara na wabunge wengi sana. 
Wanariadha wote walifurahi sana kupata nafasi hiyo adimu ya kuwaona watawala wetu wakiweka shada za maua katika kaburi la shujaa Sokoine. Ninapenda kuomba radhi kwa mapungufu ambayo yaliweza kujitokeza, na hadi sasa kuna mambo ambayo tunaendelea kuyakamilisha. Pia tunaahidi kuboresha mashindano hayo kwa kushirikiana na wahusika walio juu yetu kisheria. 


No comments:

Post a Comment