Latest News

Saturday, July 12, 2014

BONDIA MAHABUSU: Cheka kizimbani kwa kujeruhi

BONDIA nyota wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka (30) maarufu kama SMG, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro kujibu shitaka la kujeruhi.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Said Msuya, ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa polisi, Aminatha Mazengo, kuwa Cheka alitenda kosa hilo Julai 2, majira ya jioni eneo la Vijana Social Hall, Manispaa ya Morogoro.

Mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa bila halali huku akijua kuwa ni kosa kisheria, Cheka alimpiga ngumi kichwani na tumboni mtu aliyefahamika kwa jina la Bahati Kamanda na kumsababishia maumivu.
Baada ya kusomewa shitaka, Cheka alikana kutenda kosa hilo hivyo kesi hiyo ilihairisha hadi Julai 23, mwaka huu itakapotajwa tena.

Cheka yuko nje kwa dhamana ya sh. milioni 1 kwa wadhamini wawili ambao walisaini dhamana hiyo huku upelelezi wa kesi hiyo ukiwa umekamilika.

CHANZO: Tanzania Daima


No comments:

Post a Comment