Latest News

Tuesday, July 1, 2014

SHABANI HIKI: Ninaimani timu ya riadha itailetea heshima Tanzania

Timu ya wanariadha waliokuwa Ethiopia kwa mazoezi ya maandalizi ya mashindano ya Jumuia za Madola imerejea nchini jana. Katikati ni kocha aliyefuatana na timu Ndg. Shabani Hiki.
Wanariadha hao waliowasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere waliahidi kuiletea heshima Tanzania kwa kuzoa medali katika mashindano yatakayofanyika Glasgow Scotland mwishoni mwa mwezi huu wa July.
Mwanzoni mwa mwezi June mwaka huu serikali ilitoa fedha za makambi kupitia wizara ya Mambo ya Nje katika harakati za kuinusuru Tanzania kupata medali katika mashindano hayo ya Commonwealth Games yajulikanayo pia kama "Family Games" zinazoshirikisha nchi zote zilizowahi kuwa chini ya himaya ya Uingereza.

No comments:

Post a Comment