Benki ya Azania yadhamini Kids Run Dar
RC Makonda akishuhudia makubaliano NA ESTHER GEORGE, DAR ES SALAAM BENKI ya Azania imeingia makubaliano na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kuendesha mashindano ya riadha kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 16 yajulikanayo kama Kids Run Dar es Salaam yatakayofanyika Juni 5. Hafla ya makubaliano hayo ilifanyika jana na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Benki hiyo imewekeza shilingi milioni 130 kwa ajili ya mbio hizo. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Azania, Godfrey Dimoso, alisema benki hiyo inamilikiwa na Watanzania na wamejitosa kudhamini mbio hizo baada ya kukubaliana na RT. “Hili kwetu ni tukio la kihistoria kwa kuwa benki yetu ni ya kwanza kudhamini riadha tukiwa sekta binafsi, hivyo tumekubaliana na wenzetu wa RT kushirikiana katika hilo,” alisema Dimoso. Kwa upande wake, Makamu wa Kwanza wa Rais wa RT, William Kalaghe, alisema ni mara ya kwanza mashindano hayo kupata wadhamini nje ya Serikali, hi...