Benki ya Azania yadhamini mashindano ya riadha kwa watoto
Mfano wa namba za ushiriki wa AZANIA BANK KIDS RUN zitakazofanyika Juni 5 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam Juni 5 mwaka huu Chama Cha Riadha Tanzania RT kinaandaa mashindano ya aina yake maalum kwa ajili ya watoto wa miaka 16 kwenda chini (Miaka 3 hadi 16) ili kuhamasisha michezo kuanzia umri mdogo. Mashindano hayo yatafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 6 mchana. Zoezi la kwanza mapema siku hiyo itakuwa kugawa T/Shirts (Jezi) za kushiriki zitakazokuwa na alama ya Azania Bank Kids Run kwa washiriki wote watakaokuwa na namba za kushiriki. Usajili utaanza Alhamisi wiki hii katika matawi yote ya Benki ya Azania jijini Dar es Salaam na ofisi za Chama Cha Riadha uwanja wa Taifa. Mbio hizo zitakuwa za aina tano; watoto wa kati ya miaka 5 hadi 7 watashiriki kilomita 1, miaka 8 hadi 12 watakimbia kilomita 2 wakati wale wakubwa kati ya miaka 13 hadi 16 watakimbia kilomita 5. Wale wadogo wa miaka 2 hadi 3 watashi...