HATIMAYE WANARIADHA WAWILI WAONDOKA ALFAJIRI YA LEO; WAAMBWA WAENDE NA BUKTA NA SINGLET ZA LINING, KAMA HAWANA WAAZIME UDHAMINI WAO UMEKWAMA
Baada ya viongozi wa RT kutangulia Moscow wiki jana hatimaye wanariadha wawili wameondoka leo kwa kutumia shirika la ndege ya Uturuki (Tarkish Airlines) kwenda Moscow Urusi. Wanariadha hao wanaokusudiwa kushiriki mbio za Marathon ni Msenduki Mohamed na Phaustin Musa ambao pia walikuwemo katika timu iliyokwenda Olimpiki ya London mwaka jana. Kabla ya kuondoka mmoja wao alihangaika usiku na mchana kutafuta namna ya kupata kibali cha kikazi (JWTZ), jukumu ambalo lingetakiwa kusimamiwa na viongozi wa RT waliotangulia ama basi wale waliobakia ofisini. Hata hivyo siku nne zilizopita (mimi) niliongea na mwanariadha huyo ambaye alionyesha hali ya kukata tamaa kwa kile alichodai kwamba "kazi yangu ni kufanya mazoezi ili nikaiwakilishe nchi yangu kwa uwezo wangu wote, hata hivyo kwa sababu wahusika wa RT hawanipi ushirikiano itabidi nijitose kwani Tanzania ni nchi yangu pia", alisema mwanariadha huyo ambaye aliomba namba ya simu ya ofisa moja mstaafu wa jeshi amjulishe hali