RT IMEPOTEZA MWELEKEO KULIKO WAKATI MWINGINE WOWOTE
Leonard Thadeo / Mkurugenzi wa michezo May 20 th , 2012 RT walifanya uchaguzi kwa MOU ambapo walisaini kwamba baada ya siku tisini viongozi watakuwa na katiba mpya ama sivyo watakuwa wamevunja mapatano, August 20 th , 2012 siku tisini zilitimia. ( Leo tarehe 20 th 2014 ni miaka miwili kamili imepita bila katiba mpya wala mafanikio yoyote katika mchezo wa riadha zaidi ya aibu kwa taifa letu. ( Inaelezwa kwamba mwaka mzima umetimia bila kikao cha kamati ya utendaji kufanyika kama ilivyo sheria, kanuni na taratibu za lazima za BMT. ( Leo hii RT imeburuzwa mahakamani (TEMEKE) kwa kudaiwa zaidi ya TSH: 20,000,000 kwa sababu ya uzembe wa viongozi wa taasisi hiyo isiyo na katiba inayotambulika. ( Mapema mwezi huu timu za kwenda kambini nje ya nchi zilichaguliwa mezani badala ya kuchaguliwa viwanjani kwa vigezo vya kushindanishwa ili walio bora wapelekwe. Mheshimiwa waziri hata kwa macho tu hayo yanayofanywa na viongozi wa RT huyaoni,