Latest News

Sunday, May 11, 2014

Tanzania ikipitisha sheria ya uraia wa nchi mbili nitaiwakilisha Olimpiki 2020


“Endapo Tanzania itafanikiwa kupitisha katiba yake mpya inayosukwa hivi sasa nchini humo mimi nitafurahi kujumuika na ndugu zangu wa damu kuiwakilisha nchi hiyo katika Olimpiki 2020”
 
“Mimi ni mzaliwa wa Riverside, California, Marekani, kuzaliwa kwamgu hapa kulitokana na baba yangu kuja Marekani kama mwanafunzi 1993 na kwa mapenzi yake akamleta aliyekuwa rafiki wake ambaye ndiye mke wake na ndiye mama yangu hivi sasa”

“Alimtafutia nafasi ya kuja kujiendeleza kimasomo na ndipo mimi nikazaliwa na wawili hao kutokana na mazingira hayo, nilipelekwa Tanzania nikiwa na miaka miwili nikakaa kwa miaka mitano na hata shule ya msingi nilianza Arusha ambapo baadaye wazazi wangu waliamua nirudi kupata elimu Marekani”

“Marekani ni nchi yangu ya kuzaliwa ila Tanzania ni nchi yangu kiasili (My ancestral home), ninaipenda sana Tanzania na hata ninaposhiriki mashindano ya shule hapa California huwa wenzangu wananiitaga Tanzanian boy”

CHANZO: Haya ni maneno yake Sydney Wilhelm Gidabuday mwenye miaka 17 jana huko California baada ya kushinda mashindano muhimu katika ligi ya kishule jimboni hapo! No comments:

Post a Comment