Tanzania ikipitisha sheria ya uraia wa nchi mbili nitaiwakilisha Olimpiki 2020
“Endapo Tanzania itafanikiwa
kupitisha katiba yake mpya inayosukwa hivi sasa nchini humo mimi nitafurahi
kujumuika na ndugu zangu wa damu kuiwakilisha nchi hiyo katika Olimpiki 2020”
“Mimi ni mzaliwa wa Riverside,
California, Marekani, kuzaliwa kwamgu hapa kulitokana na baba yangu kuja
Marekani kama mwanafunzi 1993 na kwa mapenzi yake akamleta aliyekuwa rafiki
wake ambaye ndiye mke wake na ndiye mama yangu hivi sasa”
“Alimtafutia nafasi ya kuja
kujiendeleza kimasomo na ndipo mimi nikazaliwa na wawili hao kutokana na
mazingira hayo, nilipelekwa Tanzania nikiwa na miaka miwili nikakaa kwa miaka
mitano na hata shule ya msingi nilianza Arusha ambapo baadaye wazazi wangu
waliamua nirudi kupata elimu Marekani”
“Marekani ni nchi yangu ya kuzaliwa
ila Tanzania ni nchi yangu kiasili (My ancestral home), ninaipenda sana
Tanzania na hata ninaposhiriki mashindano ya shule hapa California huwa wenzangu
wananiitaga Tanzanian boy”
CHANZO: Haya ni maneno yake Sydney Wilhelm Gidabuday mwenye miaka 17 jana huko California baada ya kushinda mashindano muhimu katika ligi ya kishule jimboni hapo!
Comments
Post a Comment