JOHN STEPHEN AKHWARI ,MWANARIADHA WA KIMATAIFA ALIESAHAULIKA NA VIONGOZI WA MCHEZO HUO

 JOHN Stephen Akhwari akiwa na baadhi ya medali zake alizozipata katika mashindano ya riadha ,kutoka mataifa mbalimbali. Mzee huyo anafahamika sana kwa kauli yake aliyoitoa nchini Mexico mwaka 1968 Olympic Games kuwa "Nchi yangu haijanituma kuja kuanza mashinadano; Bali kumaliza mashindano".
 Mwanadada wa libeneke la kaskazini na mwandishi wa gazeti la nipashe Bi.Woinde Shizza akiwa kwa mzee John Stephen Akhwari wakati alipomtembelea nyumbani kwake mbulu mkoani Manyara.
Hii ndio nyumba ya mzee Akhwari mwanariadha Nguli aliyeweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania Mwaka 1968 Olympic Games huko Mexico.

Mzee John Stephen Akhwari akiwa amepozi sebuleni kwake
 
Na Woinde Shizza, Arusha
JOHN Stephen Akhwari ni miongoni mwa wanariadha wenye historia kubwa
hapa nchini kutokana na umahiri wake katika mchezo huo.

Akhwari anakumbukwa sana katika Michezo ya Olimpiki kutokana na kauli
yake ya kizalendo aliyoitoa wakati aliposhiriki mbio za marathoni
katika Michezo ya Olimpiki iliyofanyika huko Mexico mwaka 1968.

Kwanini ANAKUMBUKWA?:
Wengi wamajiuliza mkongwe huyo wa riadha kwanini anaendelea hadi leo
kuwemo katika vitabu vya historia ya michezo ya Olimpiki, ambayo
hufanyika kila baada ya miaka minne?

Mwanariadha huyo mstaafu kwa sasa anakumbukwa sana kutokana na kauli
yake aliyoitoa baada ya kumaliza mbio hizo za marathoni licha ya
kutumia saa nyingi zaidi ya washiriki wengine waliomaliza mbio hizo.

“Nchi yangu (Tanzania), haijanituma kuja kuanza mbio ila imenituma
kuja kumaliza mbio, “alisema Akhwari baada ya kuulizwa na waandishi wa
habari sababu za kumaliza mbio hizo huku akivuja damu miguuni badala
ya kujitoa.

Kauli hiyo hadi leo imekuwa ni kitu cha kuwatia moyo washiriki na
mkimbiaji huyo wazamani hadi leo amekuwa akikumbukwa na jamii ya
Olimpiki duniani kwa uzalendo wake wa kuhakikisha anamaliza mbio hizo
na sio kujitoa bila kumaliza. Kwa Maelezo zaidi Bofya hapa >>>

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga