WAKATI NIKITOA SHUKRANI KWA WOTE WALIOFANIKISHA MBIO ZA " MORINGE SOKOINE MINI MARATHON 2013" MONDULI ARUSHA.


Pamoja na shukrani zote kwa washiriki wote wa kumbu kumbu za Edward Sokoine, Gidabuday ameishukuru familia ya hayati Edward Sokoine, pia Mh. Namelok Sokoine kwa kushirikiana nae kwa karibu katika kukamilisha mchakato huo. Mwisho kabisa ametoa shukurani zake za dhati  kwa ushirikiano wao wa karibu na wa dhati kutoka kwa WAZALENDO 25 BLOG na ASILI YETU TANZANIA BLOG.
Bw. Wilhelm Gidabuday (kulia mwenye koti ya bluu ) akiwa na mwanariadha wa kimataifa Bw. Phaustin Baha Sulle wakisikiliza kwa makini na  kuhakikisha zoezi la utoaji wa vyeti kwa washindi wa riadha unafanikiwa.
Gidabuday aliyasimamia kidete kuanzisha na kuratibu mbio za "Edward Moringe Sokoine Mini Marathon 2013" ambayo imeungwa mkono na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Dr. Jakaya Kikwete aliyeahidi kuwa mwakani atakuwa mgeni rasmi katika full Marathon ya kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine katika kutimiza miaka 30 toka afariki tarehe 12/4/1984 na kuzikwa kwake Monduli, Mkoani Arusha. 
Gidabuday amewashukuru viongozi wote wa kitaifa waliohudhuria, pamoja na viongozi wote wa riadha mkoa wa Arusha waliojumuika nae kukamilisha tukio hilo.
Baada ya tukio la kihistoria kuwekwa na mwanariadha wa zamani na mwanaharakati wa mchezo wa riadha nchini maarufu kama Bw. Wilhelm Gidabuday, yeye kama mratibu wa mashindano ya kumbu kumbu ya "Edward Moringe Sokoine Mini Marathon 2013" yaliyofanyika 12/4/2013 huko Monduli, sasa aelezea kwa kina hisia zake kuhusu tukio hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Gidabuday amemshukuru sana Mh. Dr. Jakaya Kikwete, kwa kutambua umuhimu na uwepo wa siku ya kumbu kumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine aliyefariki mnamo 12/4/1984 kwa ajali ya gari.

Pia pamoja na kumwagia shukrani zake za dhati Waziri wa Habari ,Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara, amemuomba Mh.Rais Kikwete kumuunga mkono wakati bado akiwa madarakani katika harakati  alizoanzisha za kukusanya nguvu ili kujenga kituo cha michezo cha kitaifa hapa nchini, kitakachoitwa "John Stephen Akhwari Sports Village" ambacho kitawawezesha kuwa weka wanamichezo wachanga kambini ili kuwapa mazoezi zaidi na kuzalisha wanamichezo wa kitaifa na kimataifa.


 pia aliongezea kuwa hao wanamichezo wachanga wanaopatikana katika mbio :kwa mfano za Moringe Sokoine Marathon wanatakiwa wapelekwe kwenye kambi maalum ili wapate mazoezi zaidi, ambayo sasa ndio ana muomba Mheshimiwa Rais aiwezeshe mapema akiwa madarakani.
 MSIKILIZE MRATIBU WA SHINDANO LA "MORINGE SOKOINE MINI MARATHON 2013" AKITOA SHUKRANI ZAKE KWA WOTE WALIOFANIKISHA MBIO HIZO:

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga