BARUA YA WAZI KUTOKA KWA MWANARIADHA WA ZAMANI WA TANZANIA
Nakumbuka sana wakati
nilikuwa nasoma Kibasila Secondary School pale Chang'ombe karibu na uwanja wa
chuma yaani uwanja wa taifa, kila mara nikitoka shuleni nilikuwa napita pale
uwanjani ili nikawaone wanariadha wa timu ya JWTZ na JKT wakifanya mazoezi ya
uwanjani.
Nawakumbuka wakina
Gwangwai, Kijuu, Ndemandio, Francis John na wengineo ambao walikuwa wakifanya
mazoezi ya mbio za mita 10,000, walikuwa wakipiga mita 400x20 wanapunzika kwa
kujogi mita 200 na walikuwa wakizipiga sekunde 60 kila moja na mbili za mwisho
walikuwa wakizipiga kwa sekunde 56.
Upande mwingine walikuwa
Musa Luliga, Kijuu na Marwa kwa jina jingine Alberto Juantorena wanapiga mita
300x15 walikuwa wanazipiga kwa sekunde 36 na ya mwisho wanaileta kwa sekunde
34.
Hawa jamaa zetu walikuwa
hawapati mialiko tuu, wao walikuwa wanasubiri michezo ya majeshi, nina hakika
kama wangepewa nafasi ya kwenda Oslo, Berlin au Stockholm Grand Prix wangefanya
maajabu kabisa.
Jamani tuwakumbuke hawa ndugu
zetu kwa kuwa wanamichezo wenye viwango vya juu sana, Pia mavazi yao yalikuwa
makuchi kuchi ya kampuni Ya UMBRO na raba za Bata wakati huo au yale mabuti
laini ya jeshi kutoka jeshi la China wakati huo.
Wakati wa mashindano ya
taifa ikipigwa mita 10,000 waliokuwa wakiita mbele walikuwa Gwangwai, Francis,
Ndemandoi na wengineo kutoka JWTZ tuu. Mita 1500 alikuwa Kijuu, na mita 800
alikuwa Alberto Juantorena.
Kwenda kukimbia Zanzibar
ilikuwa starehe tuu, maana uwanja wao ulikuwa wa kisasa.
Je, RT ina mpango gani
ya kuwaalika wakimbiaji wetu wa zamani ambao bado wako hai kwenda kwenye
mashindano ya taifa mwaka huu?, Ni muhimu tukumbuke na
pia RT ingeanzisha chumba au sehemu ya kumbukumbu ya wachezaji hawa muhimu kwa
taifa.
Kuna wachezaji wengi tuu
ambao wameitangaza nchi yetu, nitata wachache lani kama kuna mtu anawafahamu
wengine ongeka majina kwenye orodha;
Agapius Masong, Mohamed
Rutiginga, Kijuu, Francis John, Gwangwai, The Shahanga brothers, Alphonce Swai,
Timothy Kamili, John Haigaimo, Petro Meta, Mrashani, Simon Peter, The Naali
brothers, Sambu, Umbe, John Yuda na wengine wengi tuu ambao wamesahaulika.
Kuna umuhimu ya kufufua
mchezo huu mpendwa wa riadha maana wengine ndio unatupa chakula mpaka leo.
Nitaendelea siku
nyingine,
Jimmy.
Comments
Post a Comment