JUMA IKANGAA: “The will to win is nothing without the will to prepare”

Juma Ikangaa
 Juma Ikangaa ni kati ya wanariadha wachache sana duniani waliodhaminiwa na kampuni moja ya viatu kuanzia mwanzo wa harakati zake za riadha hadi kustaafu kwake bila kuhama hama kimasilahi. Nchini Japan Juma Ikangaa anafahamika kuliko hata viongozi wakubwa wa nchi kutokana na uaminifu mkubwa aliouwekeza wakati akishiriki riadha chini ya udhamini wa kampuni ya vifaa vya michezo ya ASICS ya Japan.

Mwaka 1984 katika Olimpiki ya Los Angeles California, kwa heshima ya Juma Ikangaa, kampuni ya vifaa vya ASICS ya Japan iliipatia timu ya Tanzania vifaa vyote kwa timu nzima ya Tanzania, kati ya vifaa vingi vilivyotolewa na kampuni hiyo ni pamoja na (track suits 1,000) ambazo kwa sasa Riadha Tanzania haiwezi kupata kutokana na sura mbaya iliyojengeka baada ya makampuni mawili ya PUMA na LINING kuhujumiwa na viongozi wa RT na TOC ambao baadhi yao hadi sasa wapo katika uongozi wa vyama hivyo. 'Ndiyo maana hata leo huko Morogoro wanariadha chipukizi wanakimbia peku hali makocha na viongozi wakivalia sare safi zenye kumeremeta bila ya wao kuwa na uzalendo kwa vijana ambao ni taifa la kesho'.

SOKOMOKO LOS ANGELES 1984: Kabla ya vifaa kuletwa moja kwa moja Los Angeles, Juma Ikangaa (kanali mstaafu kwa sasa) aliongea na viongozi wa TOC wakati ule ambao walikuwa M/Kiti Rafael Kubaga na Katibu Mkuu Erasto Zambi (marehemu kwa sasa) ambapo alikubaliana nao kwamba wataandika barua Japan kuomba vifaa. Barua iliandikwa na wajapani wakapeleka mzigo Los Angeles; ila tatizo lilitokea ghafla kwa wakubwa hao kubadili mawazo na kusema "hatutaki ASICS tutatumia ADIDAS. 'Tafakari usaliti huo'!.

Mwanariadha huyo anayekumbukwa duniani kote kwa msamiati aliowahi kuusema akiwa New York 1989 "The will to win is nothing without the will to prepare" hakuyumbishwa na kigeugeu cha timu ya Tanzania, yeye alitumia ASICS wakati wenzake wakitumia ADIDAS. "Juma Ikangaa is the most loyal competitor of all time, he never lets anyone down". Mjapani moja aliwahi kuniambia. Mzee Ikangaa hakubabaika bali aliagiza vifaa vile viletwe Tanzania na hatimaye akagawa bure kabisa kwa wanariadha chipukizi ambao wengi wao walikuwa majeshini. "Nilipewa bure vifaa kwa ajili ya timu ya nchi yangu; walipokataa mimi nikatoa bure kwa wanamichezo waliopo majeshini" alisema Juma Ikangaa.

MASWALI MAZITO: Kitu gani kinaweza kumfanya kiongozi mwenye dhamana ya timu ya taifa kukataa pisi 1,000 za vifaa vya michezo na kukubali vifaa vichache?. Kama siyo masilahi yake mwenyewe basi ni nini?. Na je ni kwa nini RT imefanya kila aina ya juhudi ili kumweka kando Juma Ikangaa?. Mimi najiuliza ni kwa nini Ikangaa aliyeitendea nchi hii mengi yasiyohesabika awekwe kando?. Achilia mbali sisi wadogo tunaoonekana kuwa maadui eti kwa sababu hatuogopi kusema ukweli.

Tanzania haitamsahau Ikangaa kwa sifa na uzalendo wake pale ambapo ameweza kuitumikia nchi yake katika michezo na pia ndani ya jeshi (JWTZ). Leo hii laiti Ikangaa angekuwa na nafasi ndani ya RT ama TOC tusingekuwa na tatizo la kupata udhamini katika makampuni ya kimataifa kama ASICS na mengineyo duniani. Hapana shaka ipo siku watanzania watasema "Hatukutaki wewe fisadi; bali tunamtaka huyu mzalendo.". HABARI ZA KANALI MSTAAFU JUMA IKANGAA ZITAENDELEA SIKU ZIJAZO.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga