KAMANDA (RT) ATOKA NDUKI MOSCOW, ASEMA “TUMESHINDWA”



Rais wa chama cha riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka amerejea Tanzania wakati wanariadha wawili wakiwasili Moscow tayari kwa mashindano. Kiongozi huyo aliyetangulia siku kadhaa kabla ya wachezaji amerudi akiwa na hasira isiyo na kifani, akizilaumu vyombo vya habari kwa kile alichodai kwamba “wanahabari wanawasikiliza watembea miguu wasio na tija katika mchezo wa riadha na kuwaacha wao wenye akili zao”. Pia alinukuliwa akimwaga lawama kwa makampuni ya kitanzania kwa kukataa kudhamini chama cha riadha. “Tumeandika maandiko mengi kwa robo tatu ya makampuni nchini, lakini hamna hata kampuni moja iliyokubali” alihoji Mtaka wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam jana.

Sababu ya makampuni kukataa: Wakurugenzi wa makampuni wanajali sheria ambapo kabla ya kuidhinisha udhamini katika taasisi yoyote,  ‘cross checks na double checks’ hufanyika kwanza, ambapo kasoro zikipatikana udhamini hautolewi.  Chama cha Riadha hakikufuata katiba wakati wa uchaguzi mkuu, hivyo viongozi waliopo wana tatizo la kisheria.  Mheshimiwa anashindwa kuelewa hilo vipi ikiwa yeye ni mwenye akili kama alivyodai jana mbele ya waandishi wa habari?.  ‘Kama hakujua basi leo ajue’ kwamba makampuni ya kizalendo yanasikiliza maoni ya wadau na kuyafanyia kazi, hivyo namshauri bosi wa RT apunguze jazba bali afuate sheria na kama haelewi somo aachie ngazi maana anayo shughuli nyingine muhimu aliyopewa na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makacho wa Jamaica: Rais wa RT amekiuka kanuni, taratibu na sheria ya vikao vya RT kwa kuja na wazo lake la wajamaica na kutoa maamuzi ya taasisi (RT) bila kukaa na kamati ya utendaji kujadili swala la makocha wa Jamaica. Kwanza nani kasema Tanzania hatuna makocha?. Miaka ya 1980/1990 serikali ya Tanzania iligharimia mafunzo ya makocha wengi wazalendo ambao leo hawana kazi, hivyo leo yeye aende Moscow na kurudi na uongo wa kisiasa kuhusu wajamaica?. TANZANIA MAKOCHA WAPO, YEYE TU NDIO HAJUI HILO KUTOKANA NA YEYE KUWA MGENI KATIKA TASNIA YA MCHEZO WA RIADHA

RT wanapata hela kutoka IAAF: RT wanasahau kwamba watanzania tunajua kuhusu $15,000 kwa mwaka sawa na TSH: 24,750,000/ ambazo bado hazijatolewa taarifa ya mapato na matumizi yake, yeye analalamika na kutamani RT idhaminiwe kwa lazima?, Itabidi sasa afahamu kwamba 'Tanzania ya leo siyo ile inayokumbatia ufisadi' lazima afikiri sana. WATANZANIA TUNATAKA MEDALI SIYO MAKOFI MATUPU NA LAWAMA ZA KIBABE, ‘kamanda wa vita akikimbia vita askari wafanye nini?.

Wanariadha wawili Phaustin Musa na Musanduki Mohamed ndio pekee watakaotutetea Jumamosi ya tarehe 17 Agosti 2013 (15:30 Moscow Time Zone) bila kamanda wao kuwepo kupiga makofi. Hata hivyo wamesema “tutatetea Tanzania yetu kwa nguvu zetu zote”. WATANZANIA TUUNGANE PAMOJA KUWAOMBEA.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga