KATIBA YA RT ILIYO KWAMA NA ATHARI ZAKE: NI JINSI GANI TAIFA LINGEHUJUMIWA; PONGEZI KWA USIKIVU WA BMT NA DEONIZ MALINZI

M/Kiti w BMT Deoniz Malinzi
Hivi karibuni viongozi wa Chama Cha Riadha nchini (RT) walijaribu kwa njia zote 'hops and hooks' kupitisha katiba ambayo ingebeba masilahi yao binafsi na siyo masilahi ya taifa la Tanzania. Hata hivyo harakati za wadau wenye taaluma na uzoefu mkubwa wa mchezo wa riadha uliweza kuweka "STOP" katika jitihada hizo zilizovaliwa njuga na baadhi ya viongozi wa RT ambao waliwekwa na TOC na hadi sasa viongozi hao wachache wa juu wa RT bado wanatembelea viatu vya TOC.

Deoniz Malinzi: Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) alitekeleza wajibu wake vizuri kwa kusikia vilio vya wadau, hatimaye aliangaza macho kupitia rasimu hiyo iliyojaa mbegu za 'ubinafsi' na kuamua kuzuia sheria hiyo isipitishwe hadi marekebisho kadhaa ifanyike. 'Hongera mzee Malinzi' kwa kujali haki na usawa ambao ndiyo chimbuko la amani na ustawi wa jamii na taifa letu la Tanzania.

Vipengele vya kijambazi katika rasimu: Mtanzania anayehubiriwa usawa, haki, demokrasia na utaifa afikirie vipengele vifuatavyo; Katiba iliyoandaliwa na viongozi hao wasio na chembe hata kidogo ya "UTAIFA KWANZA" walipigia debe vipengele vifuatavyo; vichache kati ya vingi ndani ya rasimu:

 (1)"Kamati ya Utendaji watapiga kura" MAELEZO YANGU: Kwa kawaida katika kikao chochote cha uchaguzi kinachozingatia demokrasia kamati ya utendaji huwa 'inajiuzulu' muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu. Je haki hiyo ya wao kujipigia kura inatoka wapi?, iweje 'yeye awe na kura ndani ya kikapu wewe usiwe nayo', mkuu wa wilaya mzima hili halitambui vipi wakati yeye ana wajibu wa kulinda demokrasia?.

(2)"Kutakuwa na Mjumbe wa Kudumu" MAELEZO YANGU: Mjumbe wa kudumu tafsiri yake ni nini?, je kwa nini viongozi wa vyama vya siasa na wa serikali hawadumu?, kidemokrasia uongozi wa kudumu ni 'dictatorship' na kipengele hicho hakina tafsiri hata kidogo ya kidemokrasia.

(3)"Uongozi usiwe na Kikomo" MAELEZO YANGU: Watanzania tunajua kwamba nchi zote zinazofuata utawala bora wa kidemokrasia unazingatia uongozi wa awamu, Tanzania yetu inaruhusu uongozi wa awamu mbili katika uongozi wa juu wa nchi. Je tafsiri yao viongozi wa RT ni nini?. Na katiba ya RT iliyowekwa kando katika uchaguzi uliopita imetamka wazi kwamba uongozi ni wa awamu mbili tu.

(4)"Kutakuwa na Mjumbe Moja tu wa mkoa mwenye haki ya kupiga kura" MAELEZO YANGU: Katiba ya sasa ya RT inatamka wazi kwamba wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi ni watatu kutoka kila mkoa. Je RT sasa wanapunguza idadi hiyo kwa nini?, mahesabu yao ni hivi (Kamati Tendaji ina wajumbe 17, na wajumbe wa mikoa watakua 25, ambapo kamati ya utendaji wakila njama ya wao kurudi madarakani watajipigia kura wenyewe ambayo ni 17 na watahitaji kura 5 ambayo itakuwa kuara 22/20 tu ili warudi madrakani kwa mtiririko wao). Je hii ni demokrasia?. Na hizo kura 5 zinazohitajika watajitahidi kuwahonga wajumbe watano tu na watakuwa na uhakika wa kuendekeza ubinafsi wao daima. Hapo ndiyo mahali Malinzi amewapiga mwekeka.

(5)"Sifa ya Uongozi RT ni SHAHADA ya kwanza" MAELEZO YANGU: Je mtu ukiwa na degree ya Veterinary ataweza kuongoza michezo ambayo inahusu zaidi 'Physica Education, Sports Management na Sports Medicine?. Kipengele hicho ni kandamizi na haina maana hata tone, wanachohitaji ni kuwa 'specific' katika elimu na pia lazima wazingatie kwamba wanariadha waliowahi kushinda medali wanayo 'experience' ya kutosha maana wakati wa ushiriki wao wanapata 'Practical Knowledge' na wanaweza kumzidi hata Mtaka katika mbinu na uelewa wa uongozi wa RT.

MSISITIZO: Hivi ni vipengele vichache sana kati ya mengi yaliyo na makosa, ila hayo ndiyo muhimu zaidi na 'patachimbika' iwapo RT wataendeleza ubabe na jeuri ya kuwabeza wadau ambao ni wataalamu zaidi. Ifahamike kwamba viongozi wa RT wa juu wengine hata 'mbio za ngazi ya kata hawajawahi kushiriki' alafu wanadiriki kusema "wao ndio wanafahamu riadha; wengine ni watembea njia barabarani". Malinzi kaza buti kama ulivyokaza kwa TFF. 'Utuite sisi sote kila moja wetu awe na nafasi ya kutetea hoja yake vilivyo'.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga