PONGEZI: WAJUMBE WA (RT) WAKATAA MJADALA WA KATIBA HADI WADAU WOTE WAPATE FURSA YA KUIPITIA; TOFAUTI NA MATAKWA YA VIONGOZI
Wanariadha wa kimataifa wa Tanzania |
Leo Agosti 25, 2013 ilikuwa siku ya kujadiliwa na kupitishwa kwa katiba mpya ya Chama cha Riadha Tanzania (RT), hata hivyo kwa mara ya kwanza viongozi wenye nyuso za kuogopwa na wajumbe kutoka mikoani hawakuamini macho yao pale ambapo walishuhudia upinzani mkali wenye kuambatana na maswali yaliyoenda shule kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
Mjadala huo mzito ulianza pale ambapo baadhi ya wajumbe walidai kupewa 'hadidu rejea' kabla ya ajenda kuu kuanza, wengine walihoji vyema kabisa kwamba "huu ni mjadala wa katiba mpya au ni mjadala wa mabadiliko ya katiba"?. Mara ghafla viongozi hao wa RT waliozoea kubebwa ba viongozi wa TOC ambao wameegemea pande zote (RT na TOC) kwa uroho wa kimasilahi, walijikuta wakiwa hawana pa kuegemea kutokana na moto mkali kutoka mikoani. Baada ya mabishano yaliyoambatana na 'Cross Examination' RT na ndugu zao TOC hawakuwa na namna nyingine bali kunyanyua mikono na kulazimika kuahirisha mjadala unaohusu katiba hadi Novemba 30, 2013.
KULIKONI: Inafahamika kwamba uongozi wa RT umeipeleka nchi yetu pabaya, kiasi kwamba bila aibu utakuta viongozi hao wanafurahia uwepo wa mashindano ya kimataifa 'siyo kwa nchi yetu kushiriki vyema bali kwa wao viongozi kupata nafasi ya kujenga vitambi vyao'. Ushahidi siyo wa kutafutwa wala kufikirika, ni juzi tu tuliposhuhudia kiongozi wa juu wa RT akipiga makofi mjini Moscow huku akiwaacha wanariadha Musanduki Mohamed na Phaustin Musa nyuma wakihangaika kutafuta jinzi ya kuwafuta machozi watanzania. Mbali na hapo pia viongozi hao wasio na kipimo chochote 'below standard' walidiriki hata kutaka kupitisha katiba hovyo isiyo na mashiko. 'NI SAWA NA WIZI WA MCHANA' yaani hata hawakujali kuandika vipengele kama "Kamati ya Utendaji iwe na haki ya kupiga kura, eti awepo mjumbe wa kudumu, pia mpiga kura awepo moja tu katika kila mkoa nk". HUO NDIO WIZI ULIOKATALIWA NA WAJUMBE KUTOKA MIKOANI; HONGERA SANA WAJUMBE KWA KUZINGATIA "UTAIFA KWANZA".
SHUKURANI ZAIDI: Wadau na wataalamu halisi wa mchezo wa riadha wamempongeza sana mweyekiti wa BMT Deoniz Malinzi kwa jitihada zake za kusimamia mabadiliko chanya ya mchezo wa riadha sambamba na michezo mingine yote yaliyopo chini ya BMT. Kuna tetesi kwamba viongozi mafisadi wa TOC walishajipanga kutumia kiasi chochote cha fedha kuhakikisha katiba hii ya kihuni inapia 'IWAPO' Deoniz Malinzi asingejitokeza katika ukumbi wa mkutano. "Sasa imethibitika kwamba mtetezi wetu sisi wapenda michezo ni Deoniz Malinzi pekee" alisema mjumbe moja kwa njia ya simu. Aliongeza kusema "Laiti Malinzi angekuwepo Dodoma wakati wa uchaguzi wa TOC uhuni ule wa kuwafukuza wajumbe wa BMT ndani ya ukumbi usingefanyika, hata hivyo huu ni mwanzo mzuri" alimalizia mjumbe huyo wa RT.
Mkutano huo ulifanyika mara baada ya mashindano ya Riadha Taifa kumazilika hapo jana mjini Morogoro ambapo msukumo wa mashindano hayo ulionekana kutoridhisha kutokana na mpangilio hafifu wa ngazi zote za shirikisho hilo dhaifu hapa nchini. 'Hata hivyo viongozi wasio waaminifu wameanza kuamini kwamba RT siyo shamba la bibi, maana wanaharakati wa michezo nchini wapo bumper to bumper nao, na wanaharakati hao hawajali nyadhifa zao serikalini'.
Comments
Post a Comment