WIZARA YA MICHEZO INASTAHILI KUWAJIBIKA KWA NANI?; VYAMA VYA MICHEZO AMA TAASISI ISIYO YA KISERIKALI?



FABRIZIO CALDARONE
LEONARD THADEO


Hivi karibuni Chama Cha Tennis Tanzania (Tanzania Tennis Association) kilipitisha katiba yake na kufanya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wake baada ya miaka mingi ya udikteta ndani ya chama hicho. Hata hivyo baada ya muda mfupi wa furaha kwa wapenzi na wadau wa mchezo huo nchini, mzimu wa uongozi wa zamani umeendelea kuikumba taasisi hiyo muhimu katika michezo.

Katibu wa zamani (aliyelazimika kujiuzulu) INGER NJAU na mwenzake FABRIZIO CALDARONE wamekuja na taasisi yao mpya ya ATP TENNIS FOR CHARITY ambapo huko ulaya kuna taasisi inayofahamika kwa jina la TENNIS FOR AFRICA, “ taasisi hizo mbili zenye majina tofauti lakini zenye wanachama haohao (Inger Njau na Fabrizio Caldarone) zina harufu ya utata” alisema mjumbe moja ambaye hakupenda jina lake litajwe. “Lakini utata zaidi ni pale ambapo mkurugenzi wa michezo nchini LEONARD THADEO alipowapa kibali cha kuendesha "shughuli za Tennis" kwa viongozi hao wa kigeni na kutotoa fursa na ushirikiano stahiki kwa chama chenye dhamana ya kusimamia mchezo wa Tennis Tanzania” mtoa habari huyo aliendelea kuelezea.

INGER NJAU
UCHUNGUZI ZAIDI: Hata hivyo katika mkutano wa kamati ya utendaji wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni mengi yaliibuka kuhusu uongozi uliopita, ambao kimsingi kiongozi huyo wa zamani aliyelazimika kujiuzulu akishirikiana na raia mwingine wa kigeni ndio hao ambao taasisi yao inayofanya kazi sawa na majukumu ya Tanzania Tennis Association. Ilibainika kwamba siku tatu (3) tu kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika (19/6/2013) uongozi huo wa zamani ulichota fedha benki (withdrawal) kiasi cha  US $: 12,000 sawa na TSH: 19,800,000/= pamoja na fedha zingine za kitanzania ambazo idadi yake haikufahamika mara moja, kimsingi waliamua kufanya hivyo kwa sababu walijua kwamba uongozi wao unaelekea mwisho, na kwamba uongozi mpya ukiingia hawataweza kutoa fedha hizo benki kutokana na mabadiliko ya kiuongozi.

UONGOZI MPYA: Baada ya mjadala mkali kuhusu katiba ya Chama Cha Tennis Tanzania kuvunjwa na fedha hizo zilizotolewa na uongozi huo wa zamani, kumeonekana kuwepo na mpasuko mkubwa kati ya wanaotaka kuacha kuhoji fedha zilizotolewa kinyemela dhidi ya wale wanaotaka kujua kulikoni?. “Lazima tujue sababu ya fedha hizo kutolewa, nani anawalinda watu hao?, kwa nini hadi sasa stakabadhi zote za kibenki (financial documents) hazijakabidhiwa kwa uongozi mpya kama alivyoahidi rais aliyepita kwenye mkutano mkuu wa TTA uliopitisha katiba na kufanya uchaguzi?, kama zimekabidhiwa; nani anawalinda wakwapua fedha za chama wasiwajibishwe? iweje mpaka sasa uongozi mpya hauna majibu?” alihoji mtoa habari huyo aliyeongea kwa uchungu kwa kujali masilahi ya mchezo wa tennis. "KWA KUWA INGER NJAU AMENUKULIWA AKISEMA KUWA ALIPEWA RUHUSA NA LEONARD THADEO" JE MKURUGENZI HUYU WA MICHEZO NCHINI ALISTAHILI KUTOA KIBALI CHA N.G.O KUFANYA KAZI AMBAZO NI MAJUKUMU YA CHAMA CHA TENNIS TANZANIA?. “Je mkurugenzi huyo wa michezo anafahamu Conflict of Interest kati ya taasisi hizo mbili za kigeni na chama chenye dhamana ya mchezo husika?, ama pengine mkurugenzi hajali vilio vya watanzania bali anajali vilio vya wageni kwa sababu anazozijua yeye?. Au pengine mkurugenzi huyo anayo masilahi binafsi na taasisi hiyo inayofungamana na taasisi iliyopo Ulaya?.


UTAIFA KWANZA: Muda sasa umefika wa viongozi wenye mtazamo wa kimasilahi kusemewa waziwazi sababu kama ni swala la mkurugenzi wa michezo nchini historia yake ni ‘ndefu na  mbaya balaa’!. Mfano mzuri ni pale mkurugenzi huyo alipokuwa na uhusiano wa kimasilahi na TOC ambapo wakati wa London Olympics bosi huyo wa wizara aliona London ni rahisi kufika kuliko Kibaha ambapo wadau walilalamika aende kuhakiki hali ya kambi ya Riadha na hakwenda, lakini London alikwenda haraka kuliko Super Sonic . ‘Itakuwa ajabu kama mkurugenzi mmoja ataendelea kuendekeza dalili za kifisadi wakati waziri na naibu wake wakitulia kila kukicha’. WAZIRI SIKILIZA VILIO VYA WADAU WA MICHEZO; MAANA WAO NI WATU NA SIYO VYURA;  BINADAMU MWENYE AKILI TIMAMU HAWEZI KULIA WALA KULALAMIKA BURE. Upande wa riadha wadau wamelalamikia ufisadi uliosababisha makampuni mawili ya kimataifa (PUMA na LINING) kutuita matapeli, mkurugenzi anayetajwa anafahamu mwanzo mwisho yaliyojiri kuhusu makampuni hayo mawili, kama hahusiki basi anawalinda waliohusika, AMBAPO KISHERIA KUHUSIKA AMA KULINDA WALIOHUSIKA NI KOSA LA JINAI.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga