ANDREA SAMBU SIPE: MWANARIADHA PEKEE TANZANIA ALIYETWAA UBINGWA WA MBIO ZA NYIKA ZA DUNIA 1991

Andrea Sambu Sipe (kushoto)
Ilikuwa tarehe 24 March 1991 mjini Antwerpen nchini Ubelgiji ambapo Tanzania ilijipatia historia ya kwanza na ya pekee kwa Andrea Sambu Sipe kushinda mashindano hayo makubwa ya nyika duniani.

Siyo Bayi wala Nyambui ambao wanatanda magazetini kila siku, hakuna mwingine aliyewahi kushinda ubingwa wa dunia wa mbio za nyika (World Cross Country Championships). Andrea Sambu pia aliendeleza moto pale ambapo alivunja rekodi ya dunia ya vijana ya meta 3,000 nchini Italia. Pia Sambu ana rekodi nzuri ya mbio za marathon ambapo alikimbia masaa (2:09:52) Seoul Korea 2004.


Kama ilivyo kauli mbiu ya blog hii "Utaifa Kwanza", madhumuni makubwa ya kuibua historia njema zilizoletwa na watu wema ambao taarifa zao zinafichwa kwa makusudi ya kuendeleza sifa za watu fulani; nimedhamiria kuibua mazuri yote yaliyofanywa na watanzania wenye nia njema kama Andrea Sambu, Phaustin Baha Sulle na wengine wengi moja baada ya mwingine.

Wiki iliyopita Sambu alishiriki mashindano ya Safari Marathon na kufanikiwa kupata nafasi ya tano kwa kukimbia dakika 63 (1:03) muda ambao ni wa kimataifa. Sambu amekuwa mtanzania aliyedumu kwa muda mrefu katika riadha ambapo amekuwa katika 'hili game' kwa zaidi ya ROBO KARNE na bado anatarajia kutuwakilisha.


Katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon ya mwaka huu Sambu alikamata nafasi ya tano ila alifanyiwa hujuma na John Bayo ambaye aliwahi kuwa manager wake katika mbio za Ulaya, hivyo kuna kipindi ambacho Sambu aliona ni muda muafaka wa kuhamia kwa manager mwingine, kitu ambacho kilimchanganya Bayo na kuweka uhasama hadi wa kudumu.

Haiwezekani mwanariadha akapewa karatasi inayoonyesha amekuwa wa tano, alafu akapelekwa chumba cha 'Doping Control' kama hakuwa katika top ten!. Sambu alizubaishwa ndani ya Doping Control Area wakati mafisadi wakibadilisha matokeo haraka maana yule aliyepewa nafasi ya tano aliwalipa 'The team of Syndicates' asilimia kadhaa ya ile fedha ya ushindi.

Wanariadha wote wa sasa na wa zamani tulifanya bidii kutaka ufafanuzi lakini RT nao wakapiga kimya, kwanza tulihoji iweje namba tano apewe mtu asiyefahamika katika viwanja vya riadha?. 

LIOSHIYE MOIKAN ndiye aliyepewa nafasi ya Sambu, jina ambalo halifahamiki wala RT hawakuwa tayari kulizungumzia maana ni uhuni uliofanyiwa taifa zima siyo Sambu tu wala wanariadha pekee. Hivyo Sambu akanyamaza na kuendelea na mazoezi, lakini RT hili lina maana gani?.

Uongozi haramu: Pamoja na RT kuwa madarakani kinyume cha katiba na sheria za BMT pia wameshindwa kutetea haki za wanariadha ambao walipeperusha bendera katika mashindano ya kimataifa kama Sambu. 

Kwa kutofuatilia swala la Sambu kudhulumiwa nafasi aliyoshinda kwa jasho lake, wameliingizia taifa hasara na aibu. Yote hayo ni sababu ya wivu na uhasama wa mtu moja tu!. All for that for what?.

Taarifa za utata wa matokeo: Tulimjulisha Mtaka na Nyambui lakini wakapuuza, badala yake walimpa promotion John Bayo kupeleka timu ya Cross Country Poland ambapo pia kuna utata ambao hivi sasa tunalifanyia utafiti kubaini je ni wanariadha wangapi walikwenda Poland, na kama idadi siyo waliotaja wao basi taifa liwafikirie RT na John Bayo vipi?.

 'Tukikamilisha uchunguzi wetu tutaanika hadharani bila kuogopa kuku wala jogoo'. UTAIFA KWANZA NDIYO NGUZO YETU MUHIMU. Hongera Sambu; Tupo Pamoja.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga