PHAUSTIN BAHA SULLE: MWANARIADHA ALIYEKATAA KUPOKEA ZAWADI BILA BENDERA YA NCHI YAKE KUPEPEA MBELE YAKE AKIWA VERACRUZ MEXICO
Mwanzo wa mashindano ya dunia mjini Veracruz Mexico, Tanzania ilipata medali ya Fedha kupitia mwanariadha Phaustin Baha Sulle |
Ilikuwa katika mbio za Lisbon Half Marathon 2000 ambapo wanariadha kutoka Kenya, Ethiopia, Moroco, Tanzania, Ulaya, Marekani na Asia walipokutana nchini Ureno kushiriki mashindano hayo makubwa duniani.
Phaustin Sulle nyuma ya Paul Tergat |
Paul Tergat wa
Kenya aliyekuwa akishikilia rekodi ya dunia ya nusu marathon kwa wakati huo
alikuwepo katika mstari wa kuanzia mbio.
Wanariadha wote walikuwa wakimtazama Tergat na wakenya wenzake, hawakujua kuna kijana chipukizi kutoka Babati Tanzania ambaye hakujali nani yupo, yeye alisubiri kwa hamu mbio zianze. Muda mfupi baadaye Paul Tergat alijikuta akitolewa jasho na Phaustin Baha Sulle kuanzia kilomita ya kwanza hadi ya kumi.
Wanariadha wote walikuwa wakimtazama Tergat na wakenya wenzake, hawakujua kuna kijana chipukizi kutoka Babati Tanzania ambaye hakujali nani yupo, yeye alisubiri kwa hamu mbio zianze. Muda mfupi baadaye Paul Tergat alijikuta akitolewa jasho na Phaustin Baha Sulle kuanzia kilomita ya kwanza hadi ya kumi.
Ndipo sasa Tergat alipotumia uzoefu wake kumdhibiti Sulle
hatimaye Tergat alishinda mbio hizo kwa umbali mdogo sana kati yake na Phaustin
Baha Sulle. Tergat alikimbia dakika 59:34
na Sulle nyuma yake kwa 59:36. Rekodi hiyo ilimfanya Sulle kuwa mtanzania
wa kwanza kukimbia chini ya saa moja na pia alivunja rekodi ya vijana ya dunia
papo hapo.
Miezi sita baadaye Tergat
na Sulle walikutana mjini Veracruz Mexico katika mashindano ya
dunia ya nusu marathon ambapo Tergat kwa mara nyingine alitokwa jasho kwa kumshinda
Sulle kwa sekunde moja, ambapo Sulle aliiletea Tanzania medali ya Fedha. “Nilikataa
kupokea zawadi maana bendera ya Tanzania haikuwepo; wamexico waliheshimu
msimamo wangu wakasubiri bendera ilipoletwa ndipo tukakabidhiwa zawadi zetu” alisema
Sulle.
Je watanzania wanafahamu kwamba zaidi ya Bayi na Nyambui kuna walioweka historia nzuri zaidi?. ‘Imezoeleka kwamba
kumbukumbu zinazoandikwa kila mara itamtaja Bayi na Nyambui pekee wakati kuna
wengine ambao walifanya vyema na wakaamua kukaa zao kimya.
Kukaa kando ni uzalendo zaidi kuliko hao wanaotajwa kila siku ambao wamekuwa ving’anganizi
katika uongozi wa vyama vya michezo ili kujinufaisha wao wenyewe’.
Comments
Post a Comment