MTAZAMO: USHINDI WA URAIS TFF UNAKWENDA KWA JAMALI MALINZI
Jamali Malinzi |
Baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya TFF na ‘Hali Halisi’
yaani katiba ya haki sasa uchaguzi utafanyika October 27, 2013, hiyo ni baada ya wenye masilahi binafsi kushindwa
kumzuia Jamali Malinzi kugombea ‘sasa wana haha’
Mtazamo wa sasa ni kwamba wajumbe na wadau wengi wa soka
nchini wamechoshwa na ujanja ujanja mwingi uliozoeleka, mara nyingi waliopo
madarakani hutumia nguvu yao ya kiofisi
(Abuse of Power) kuwabana wanaowania madaraka kwa kulinda masiliahi yao
waliyojichotea wakati wakiwa madarakani.
Hata kama wao wenyewe hawagombei lakini watawapandikiza
vibaraka (Puppets) ambao watalinda
ule mnyororo wa kifisadi ndani ya ofisi hizo.
Shaffih Dauda
amejikuta akiporwa fedha zilizodaiwa kuwa faini na kamati iliyojiita (chombo cha juu cha maamuzi); cha kushangaza ni kwamba
chombo cha chini kilipobatilisha maamuzi, chombo hicho cha juu hakijalalamika. ‘Kitendo
kinachoashiria kuwa ni ‘ Syndicated Matter’ hivyo Shaffih akatolewa kafara.
Je wanaojitahidi kuharibu michezo Tanzania wataendelea hadi
lini? Bila shaka wapiga kura wa uchaguzi mkuu wa TFF ndio wenye dhamana ya
kuweka NUKTA ya ujanja ujanja huo kwa kuwachagua viongzi wenye kujali “UTAIFA
KWANZA”.
Comments
Post a Comment