Nyerere Day: Je Nyerere anakumbukwa kimaneno ama anakumbukwa kiukweli?


Ukisoma maneno kutoka katika "nukuu zake" utaona kwamba alichokisema nyakati zileee.. 'enzi za mwalimu' ndiyo yanafanyika kinyume na alivyokuwa akitaka; mbaya zaidi wale wanaodai kumpenda Nyerere ndiyo kwanza wanaoendekeza balaa la kuiuza nchi.

Mfano upo wazi: Hivi sasa Wilaya nyingi Tanzania tunashuhudia migogoro ya ardhi inayosukwa na wakuu wa sehemu husika, lakini uchonganishi unawakumba wafugaji na wakulima! Hivi jamani watanzania haya maneno ya mwalimu yanazingatiwa?.

Comments