Ruksa serikali kushiriki kukimbiza kifimbo cha Malkia lakini haramu serikali kuhoji ufisadi ndani ya TOC


Rais Kikwete akiwa na timu ya Olimpiki London 2012

Je serikali ya Tanzania ni serikali ya kuchezewa kihivyo na genge la mafisadi wanaijidai wao hawaguswi na serikali? 

Je raisi wetu Mheshimiwa Jakaya Kikwete atafurahia ‘kijifimbo’ cha Malkia badala ya kupewa ripoti ya USD 100,000 zilizopakuliwa India?

Kama kawaida ya sera yetu ya “UTAIFA KWANZA” tunaiomba serikali kupitia Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Wizara ya Habari, Vijana,  Utamaduni na Michezo watafakari mambo yafuatayo:

-          Kwamba TOC inauma na kupuliza; wanatabasamu kwa serikali wakati wanajiseti kwa Picture Perfect” pale tu wanapotaka kudanganya ulimwengu kwamba wao ni vinara nchini.

-          Kwamba TOC ipo radhi kumpata rais wa Jamhuri ya Muungano ajumuike nao ili wazitumie zile picha kuchota fedha ambazo wanajengea mahekalu yao watanzania tukiishia patupu.

-          Kwamba wakati wa uchaguzi wa TOC Desemba 8 2012 Dodoma TOC ilihakikisha hakuna serikali inaingia ndani ya ukumbi angalau ku-observe jinsi uchaguzi unavyofanyika; aliyekubaliwa ni ‘Share Holder’ wa TOC Corrupt Team Leonard Thadeo. Zanzibar haikushirikishwa kwa sababu ya chuki binafsi kati ya TOC na mwenyekiti wa BMZ ambaye alifungiwa nje ya ukumbi.

-          Kwamba waziri sasa anatakiwa kuwa waziri wa ukweli, aanze kuuliza maswali yatakayozaa majibu ya kitaifa; siyo kujiunga na makamati ya kijambazi jambazi eti sababu pale pana mlo!

Kama serikali itashindwa kuihoji TOC; basi watueleze sisi watanzania hela hizo nani anazitumia? ‘SISI TUNAHITAJI MPANGO UTAKAOTULETEA MEDALI YA OLIMPIKI KULIKO KIJIFIMBO CHA MALKIA’

Watanzania tujiulize hili: "Ni kwa nini wakati wa kufikiria timu ya Olimpiki iwe wapi mheshimiwa wa TOC hakuunda kamati kama aliyoiunda hivi sasa"? 

Bila shaka huo ni mchoro unachongwa na bila ya aibu TOC wanaseti mpango mzima ili raisi wa nchi aibariki UFISADI huo bila yeye kujua! Je tutaendelea kuburuzwa hadi lini?. SIKU ZA KUBURUZWA NA MAFISADI ZIMEBAKI KIDOGO SANA. 

'Ni bora mara milioni kukimbiza kifimbo cha Mwl Nyerere kuliko hicho cha Malkia maana hiyo ni USD 100,000 za mtu binafsi!


Comments

  1. Tukimbize Kifimbo cha Mwalimu kuweka Mbele Utaifa, UTAIFA KWANZA, huyo Malkia wa Uingereza na Nyerere nani Bora kwa Taifa letu, kwanini tusiwaze kufanya hivyo badala yake tunafanya Upuuzi huu?Pesa zetu hatujui nani atazifidia leo tunazidi kuongeza Up***i kama huu

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga