Sir Alex Ferguson awapa moyo Manchester United
Ferguson alistaafu baada ya kuiongoza klabu kwa miaka 27 |
Aliyekuwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema kuwa wachezaji wa Man U wanaweza kubadili mwanzo wao mbaya kwenye ligi ya Premier, licha ya kuwa pointi nane nyuma ya timu inayoongoza ligi hiyo kwa sasa Arsenal.
Ushindi mara mbili wa timu hiyo katika mechi
mbili zilizopita , ina maana kuwa upande wa David Moyes wameweza
kujikomboa kutokana na matokeo mabaya zaidi ya Man U katika mwanzo wa
ligi hiyo, kuwahi kushuhudiwa katika miaka 24 ya klabu hiyo.
Ferguson, mwenye umri wa miaka 71, alisema sio mara ya kwanza kwa
klabu hiyo kuwa na mwanzo mbaya wa msimu. Imetokea mara nyingi.
"Man U ndio klabu pekee kuwahi kutoka nyuma kwa
pointi na hatimaye kushinda ligi,'' alisema Ferguson
Ferguson, aliyesalia kuwa mmoja wa wakurugenzi
wa klabu hiyo , alistaafu kutoka katika wadhifa wa meneja mkuu wa klabu
mwishoni mwa msimu baada ya kushinda mataji 38 katika usimamizi wake wa
miaka 27.
Naye menaja mpya Moyes anakumwba na wakati mgumu
upande wa mashabiki baada ya kuanza vibaya msimu.
KUTOKA: bbcswahili.com
Comments
Post a Comment