Spoti Kizaazaa hewani TBC: Kituo chako cha televisheni ya Taifa
Ally Hozza ni miongoni mwa watoa hoja |
Ndugu wapendwa kile kipindi kinachopendwa na watanzania wengi kutokana na kuwa mstari wa mbele kutoa ukweli kuhusu kudorora kwa michezo nchini kinarudi hewani.
Spoti Kizaazaa kinarudi kwa kishindo kupitia Televisheni ya Taifa (TBC), kituo kinachobeba kauli mbiu ya "Ukweli na Uhakika". Kitakuwa kinarushwa kila Jumapili saa TATU UNUSU usiku.
Awali Spoti Kizaazaa kilikuwa kikirushwa na ITV, hadi mkataba wa muda ulipoisha ndipo kikakwama kwa muda wakati mpango mwingine mzuri zaidi ukisukwa na waandaaji wa kipindi hicho maarufu sana.
Awali mjumbe moja wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (Peter Mwita) alinukuliwa na "Private Investigator" akidai kwamba "Fedha nyingi za TOC ndio zimezima vuguvugu la Spoti Kizaazaa lililojaa genge la wahuni".
Kauli hiyo haikuwafurahisha wengi lakini sasa furaha imerudi na nukuu hizo zenye thamani ya bia mbili hazitunyimi wanaharakati wa michezo usingizi.
Kauli hiyo haikuwafurahisha wengi lakini sasa furaha imerudi na nukuu hizo zenye thamani ya bia mbili hazitunyimi wanaharakati wa michezo usingizi.
Wote mnakaribishwa kushiriki kutoa maoni yenu na pia kusikiliza maoni ya wadau wenzako.
Comments
Post a Comment