YOHANA MWILA: MWANAMICHEZO MLEMAVU WA TANZANIA ALIYE HUJUMIWA AFRIKA KUSINI
- Get link
- X
- Other Apps
Yohana Mwila |
Wachezaji hao walemavu waliowakilisha nchi yao ni pamoja na Novatus
Temba, Yohana Mwila na Juma Hamisi ambao wote ni wachezaji wa tenisi, mara nyingi hawakosekani katika viwanja vya Gymkhana Dar Es
Salaam.
Wachezaji hao mahiri walifuatana na mwalimu wao (coach) Riziki Salum
ambaye kazi yake kubwa ni kuwaongoza na kuhakikisha kwamba wachezaji
wake wanasafiri na kufika salama, wanapata malazi na chakula na pia
kuhakikisha kwamba wanashiriki mashindano na kupewa matokeo halali.
Hata hivyo uchunguzi umebaini kwamba mwalimu huyo hakufanya kazi yake
kizalendo kwani safari aliyotumwa aliibadili na kuwa safari yake ya
kutalii.
Uchunguzi umeonyesha wazi kwamba vipindi vyote ambavyo
wachezaji walipambana kuiletea sifa Tanzania kocha huyo hakuwepo
uwanjani kushuhudia na kutetea matokeo ya watanzania aliotumwa
kuwatetea.
Matokeo ya uzembe wa mwalimu huyo umeisababishia nchi (Tanzania) hasara
ya kukosa ushindi kutokana na mchezaji Yohana Mwila kubadilishiwa
matokeo ambayo alipambana hadi kufikia hatua ya robo fainali.
Yohana Mwila alitegemea kucheza nusu fainali katika mchezo wa singles,
hivyo akaendeleza mapambano katika mchezo wa doubles.
Wakati yeye
anacheza katika doubles makocha wa Afrika Kusini wakapanga njama ya
kubadili matokeo na nusu fainali ikaendelea katika uwanja wa pili huku
Yohana akipambana katika uwanja mwingine.
Lakini ghafla wakati wa chakula cha jioni Mwila alibaini kwamba fainali
za singles zimesha chezwa!, mara moja akatoa malalamiko kwa wahusika.
"Niliambia ni kweli kuna kosa limefanyika, na kwamba watarekebisha kesho
ila niliambiwa kocha wako yupo wapi?, ndiye anayestahili kutetea haki
zako" alisema Mwila kwa huzunu kabisa.
Hivyo hapana shaka kwamba kosa lilifanyika, lakini hata kesho yake kocha
Riziki Salum hakuonyesha bidii zozote na hatimaye hakijarekebishwa
kitu!. Badala yake bwana Riziki alikazania kwamba "sasa hatuna la
kufanya, labda tuwaombe wahusika watupendelee kwa siku zijazo"
alinukuliwa akisema mwalimu huyo asiye mzalendo hata tone.
Viongozi wa Paralympic mpo wapi?, au mnapenda kuwaonea vilema wenzenu wakionewa?,
ili hali mungu amewapa ninyi ulemavu, na mnafahamu uchungu wa kuwa
walemavu lakini bado mnabariki uonevu wanaofanyiwa walemavu kwa
kuto sema chochote!.
Kama hiyo haitoshi rais na katibu wa Paralympic (Johnson Jason Meela na
Iddi Kibwana) bila kujali wala kuheshimu katiba wamekaidi utaratibu wa
kufanya uchaguzi uliopaswa kufanyika 2010 ili waendelee kukaa madarakani, kitendo ambacho ni cha
uonevu dhidi ya wachezaji walemavu.
Gidabuday Sports Tourism Foundation is a Non Profit Organization based in Arusha. It's main purpose is to promote, sensitize and enforce education through sports, as well as to search and develop new talents for sports from young people from marginalized communities all over the country.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment