MAJANGA: Marekebisho ya katiba ya RT haitambui masilahi wala uwepo wa muungano kwa kuitenga Zanzibar
ZANZIBAR TANZANIA |
Augosti 25/2013 Chama Cha Riadha Tanzania (RT) kilijipanga kupitisha rasimu
ya katiba ya chama hicho Morogoro kabla ya kuwashirikisha wadau na wanariadha
waliopo mikoani.
Kwa bahati nzuri BMT waligundua tatizo na kutoa tamko la zoezi hilo
kuahirishwa hadi hapo wadau mbali mbali nchini watakaposhiriki kutoa maoni ya
vipengele vya katiba hiyo.
Pamoja na zoezi hilo kutofanyika ipasavyo hadi sasa Zanzibar imestuka na
kupinga kutoshirikishwa kwake hata katika TAFSIRI ya katiba hiyo, kitendo
ambacho kimesababisha wazanzibari kuamka na kutaka ufafanuzi kutoka kwa viongozi
wa RT.
“Zanzibar hatutambuliwi na shirikisho la riadha duniani (International
Association of Athletics Federation) halafu eti tusitambuliwe pia na Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania” alihoji mdau muhimu wa riadha kisiwani Zanzibar.
“Pia sisi wadau wa Zanzibar tunataka mgao wa fedha zinazotokana na IAAF
kwani sisi ni nchi mbili zenye mahitaji sawa maana sisi ni muunganiko wa vitu
viwili vilivyopo sawa” mdau mwingine aliongezea.
Madai ya wazanzibari yanachukua uzito wenye mashiko sababu nchi yetu hivi
sasa ipo katika mpito wa kihistoria kwa kipindi hiki cha kuandaa katiba mpya
yenye makusudi ya kuimarisha muungano wetu; hivyo haileti maana yoyote pale
ambapo vyama vya michezo vinaleta chembe chembe za utengano.
Ni muda muafaka sasa viongozi wa BMT na BMZ kukaa na kuangalia namna bora ya
kutatua hitilafu hii isiyoonekana kwa viongozi wasioheshimu hata katiba zao
wala kuona mbele.
Bila shaka M/Kiti wa BMT Deoniz Malinzi ataona umuhimu wa kuhifadhi fedha zake alizoahidi kuzitoa kwa kugharimia zoezi hilo la kupitisha katiba November 30/2013 Morogoro hadi hitilafu hizo za KERO ZA MUUNGANO michezoni zitakapowekwa sawa.
Vinginevyo posho za mikutano zitatafunwa hatimaye katiba kukwama na Tanzania ikaendelea kupata aibu kwa gharama ya siasa chafu viwanjani.
Vinginevyo posho za mikutano zitatafunwa hatimaye katiba kukwama na Tanzania ikaendelea kupata aibu kwa gharama ya siasa chafu viwanjani.
Comments
Post a Comment