Ili kuboresha riadha Tanzania ni bora tukaweka mambo kadhaa sawa kabla ya kusonga mbele bila masahihisho
John Stephen Akhwari |
Siku ya kuadhimisha uhuru wa nchi yetu ni siku muhimi sana kwa kila anayependa demokrasia, amani, mshikamano na umoja ambao baba wa taifa Mwalimu Nyerere alituachia.
Uhuru Marathon ilizinduliwa vizuri mwaka jana kwa kuonyesha picha na nukuu muhimu zilizotokea wakati nchi yetu ikiongoza dunia katika riadha, picha na nukuu za mkongwe John Stephen Akhwari zilionyeshwa.
Kati ya nukuu muhimu sana katika historia ya Olympic Games ni ile aliyoitoa John Stephen Akhwari katika mashindano ya Mexico City 1968, alisema "Nchi yangu haikunituma Mexico City kuja kuanza mbio: nchi yangu ilinituma kuja kumaliza mbio". Nukuu hiyo imejenga kitu kinachojulikana kama Olympic Spirit ambapo mzee wetu hukumbukwa na ulimwengu kila mwaka wa Olympics.
Je waandaaji wa Uhuru Marathon walikumbuka kumualika mzee wetu huyo?, tunaamini kwamba waandaaji wangethamini historia ya nchi waka - combine na historia ya Olympics kamwe wasingemsahau mzee wetu.
Hata hivyo utata uliopo ni 'kwa nini ilitangazwa kwamba Haile Gebresselassie na Edna Kiplagat watakuja kumbe sio kweli?, lakini kibaya zaidi ni pale ambapo mwaandaaji alipojaribu kupotosha kwa nguvu kwamba mshindi wa marathon ni mtanzania kumbe siyo!
Hili lilionyesha wazi kwamba mwaandaaji alitaka wakuu wa nchi waelewe kwamba mshindi ni mtanzania hadi pale wanariadha na mashabiki walipoanza kumzomea ndipo alipo badili kauli yake. JE HUO NI UUNGWANA?. Haiwezekani wanariadha wa Tanzania wasifahamu tofauti ya mkenya na mtanzania.
Na sasa kuna uvumi ambao utaendelea kuwa uvumi hadi hapo RT na waandaaji wa mbio hizo watakapotoa tamko! Uvumi wa kuwepo majeruhi na wengine kudai kuna mkenya amefariki dunia. JE HILO NI LA KWELI KWAMBA KUNA KIFO?.
Swali hilo linaelekezwa kwa RT, waandaaji na wakala wa wakenya. JE KUNA MKENYA ALIYEKUFA AMA HAMNA? Kigugumizi cha nini?.
Comments
Post a Comment