Kudumisha amani: Wanariadha wajifua kwa Mvomero Half Marathon

Anthony Mtaka/DC Mvomero na waziri Nyalandu

WANARIADHA mkoani hapa wameanza mazoezi kujiandaa na mbio za nusu Marathon za Mvomero ‘Mvomero Half Marathon’ yanayotarajiwa kufanyika Januari 12, 2013.

Wakizungumza na Tanznia Daima kwa nyakati tofauti, baadhi ya wanariadha hao walisema wameanza mazoezi mapema kwa lengo la kujiweka fiti zaidi ili kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Thobias Mkude ambaye ni miongoni mwa wanariadha chipukizi katika mbio hizo, alisema amekuwa akijifua asubuhi na jioni kwa lengo la kufanya vizuri kuuwakilisha vema mkoa wake.

“Nimeshaanza mazoezi asubuhi na jioni, lengo langu nataka kuipeperusha vema bendera ya mkoa wa Morogoro katika mashindano hayo,” alisema Mkude kuelekea mbio hizo ambazo uwepo wake ni kuibua vipaji.

Kwa mujibu wa waratibu, mbali ya vipaji mbio hizo zinafanyika kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa jamii ya wafugaji na wakulima ambao mara kadhaa wamekuwa wakiingia kwenye mapigano kutokana na mifugo na ardhi.

Source: Tanzania Daima

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga