MAZISHI: Mwanamuziki maarufu wa Congo/Zaire Tabu Ley Rochereau afariki dunia nchini Ubelgiji


Tabu Ley Rocherea

Mwanamuziki maarufu wa Kiafrika na mfalme wa muziki wa Rumba toka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Tabu Ley Rochereau amefariki dunia jana jumamosi akiwa hospitalini nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 76.

Familia ya mwanamuziki huyo imethibitisha taarifa hizo na kusema mazishi yake yanatarajiwa kufanyika jijini Kinshasa baada ya mwili wake kurejeshwa.

Tabu Ley ambaye jina lake halisi ni Pascal Sinyamwe Tabu, alizaliwa tarehe 13 Novemba 1937 huko Bandundu Magharibi mwa DRCongo, na umaarufu wake katika Muziki wa Rumba ulishika kasi zaidi katika miaka ya 1960.

Alikuwa ni miongoni mwa Wanamuziki maarufu wa Kiafrika waliobobea katika utunzi, uimbaji na uadhishi wa nyimbo.
Wakati wa utawala wa Mobutu Sese Seko, Mwanamuziki huyo alilazimika kuishi uhamishoni, na mwaka 1990 utawala huo ulipiga marufuku kusambazwa kwa albamu yake ya “Trop, c'east trop” au Too much is too much.

Tabu Ley ni miongoni mwa Wanamuziki wa DRCongo ambao wamakuwa wakijihusisha na siasa na alirejea tena nchini mwake mwanzoni mwa miaka ya 1990 baada ya kuondolewa madarakani kwa Mobutu.

Tabu Ley amekuwa katika hali mbaya kiafya toka mwaka 2008 baada ya kupata ugonjwa wa kiharusi, na amekutwa na umauti wakati akipatiwa matibabu katika hospitali moja nchini Ubelgiji.

SOURCE: kiswahili.rfi

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga