Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni: Kesho ni mbio za Karatu Sports Festival
Mbio za Karatu Sports
Festival kesho zinapigwa mjini Karatu mkoani Arusha kwa hisani ya Kamati ya Olimpiki Tanzania ikiwa ni tawi dogo
la Kamati ya Olimpiki ya Dunia.
Kwa vile ni haki kujali jitihada zozote zinazofanywa na
wadau wa michezo sina budi kuwakumbusha waandaaji mbumbumbu wanaotimukia
kuandaa ‘gemu zisizo zao’ wajifunze
angalau jambo moja ama ama zaidi ya moja katika mbio za kesho.
Kwamba si lazima uwaalike wakenya ama mataifa ya mbali ili
kuwadanganya wadhamini wakukubalie! Ikumbukwe kuwa sababu kubwa ya kuandaa mashindani
ni kuhamasisha watanzania na kuwawezesha ili kuibua vipaji vipya.
Hivyo siyo haki kutangazia umma kwamba Gebresselassie na Kiplagat wanakuja
kumbe uongo mtupu! ‘UHURU MARATHON WALITUMIA VYOMBO VYA HABARI
KUPOTOSHA UMMA MAKUSUDI’
Pamoja na mengineyo utapeli uliofanyika kwa kumnyima zawadi mshindi wa NNE mtanzania wa Mbulu (ALEX SANKA) na
kumpa mkenya zawadi hiyo, hadi leo mtanzania huyo anateseka kudai fedha
alizozishinda kwa nguvu na jasho lake mwenyewe bila kupata maji ya kunywa njia
nzima ya kilomita 42.
Pamoja na hayo kifo kilichosemwa kunyamazishwa bila tamko
lolote rasmi la kukanusha ama kuthibitisha. Athletics Kenya pia walikanusha kutoa kibali hata kimoja kwa
wanariadha wake waliodaiwa kuwa na vibali halali. Denis Malley na mwaandaaji wa Uhuru marathon aibu yao, UCHUNGUZI LAZIMA.
Nawapongeza waandaaji wa Karatu Sports Festival kwa kujali Utaifa Kwanza kwa shughuli hiyo ya kesho, ninashauri kwamba mbio
hizo zifanyike kwa mzunguko katika mikoa mbalimbali badala ya kufanyika Karatu
kila mwaka ili hamasa ya mbio hizo zienee nchi nzima.
'TANZANIA HAIPO KARATU BALI KARATU
NDIYO IPO TANZANIA; TUIPENDE TANZANIA YOTE BILA KUBAGUA KAMA RAMANI YETU ILIVYO'
Comments
Post a Comment