Nangwa mpaka California: Maisha ni safari na safari huanzia hatua moja; Tumetoka mbali na hatujui tunapoishia
Nangwa Village ndipo hatua ya kwanza ya Sydney Gidabuday ilipoanzia kabla ya kuzaliwa Marekani wakati sisi wazazzi wake tukisoma huko. Sisi wazazi wote wawili tumezaliwa na kukulia wilaya ya Hanang Tanzania. Pichani ni mimi Wilhelm Gidabuday nyuma ya baba na mama.
Pichani tukikimbia kwa nyakati tofauti mimi (baba kulia na mtoto wangu kushoto). Sijawahi kuota ndoto kwamba mtoto wangu pekee atakuja kurithi mchezo uliyenivusha kutoka kijiji cha Nangwa hadi California.
Christmas hii asante mungu kwa kumuwezesha Sydney Wilhelm Gidabuday (wa tatu kulia) kuwa kati ya wanafunzi wachache wa jimbo la California kufuzu zawadi yenye heshima tele ya kimichezo na kielimu.
Comments
Post a Comment