Riadha Kenya yawakana wakimbiaji



Dennis Malle (aliyesimama) ni wakala maarufu wa kuleta wakenya Tanzania kwa kupata 10% bila kujali uzalendo

CHAMA cha Riadha Kenya (AK), kimesema hakina taarifa za wanariadha wake kwenda Tanzania kushiriki mashindano mbalimbali mwaka huu.



Desemba 4 mwaka huu yalifanyika mashindano ya Serengeti Marathon na Desemba 8 Uhuru Marathon na kushirikisha wanariadha kadhaa kutoka Kenya ambao ilidaiwa kuwa wana barua rasmi za utambulisho kutoka AK kama inavyotakiwa kisheria.


Suala la mawakala wa Tanzania kuwachukua wanariadha wa Kenya katika mashindano mbalimbali bila kufuata taratibu limekuwa likiota mizizi huku Riadha Tanzania (RT), ikishindwa kulipatia tiba.


Katika mbio za Uhuru Marathon, zilizagaa habari kuwa mwanariadha Emily Lagat amefariki mara baada ya kumaliza mbio hizo, kabla ya wakala wake, Dennis Malle, kukanusha huku akibainisha kuwa ni mzima licha ya kwamba alikuwa majeruhi.


Malle akizungumza kwa simu kutoka Arusha, alidai kuwa Lagat aliyeshika nafasi ya nne katika mbio hizo, aliumia katika mbio hizo na kutibiwa kwa muda kisha kuendelea na mbio na kumaliza, ingawa alikuta zoezi la ugawaji zawadi limekwishamalizika.


Wakala huyo alidai kuwa wanariadha aliowaleta wote wamerejea Nairobi salama na walikuwa na mialiko rasmi, jambo ambalo AK imelikanusha.


Akizungumza na Tanzania Daima jijini hapa jana, Ofisa Uhusiano wa AK, Evans Bosire, alisema hawana taarifa zao kwani shirikisho hilo halijatoa ruhusa kwa mkimbiaji yeyote kutoka Kenya kwenda kushiriki mashindano hayo.


Alisema, kama kuna mkimbiaji amekwenda Tanzania kukimbia, hilo hawalitambui, kwani atakuwa ameenda kwa mapenzi yake mwenyewe na si kwa ruhusa ya shirikisho. Aliongeza kuwa, endapo mchezaji atapata tatizo lolote, itakuwa ngumu kwa wao kujua, kwani hawana taarifa zozote juu yao.
 
Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, alidai kuwa, kuna udanganyifu unaofanyika wa barua za ruhusa na kwamba watalifanyia kazi.

SOURCE: Tanzania Daima


Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga