SAMBU: Mkongwe wa riadha Tanzania afanikiwa kufikia kiwango cha kuwakilisha Tanzania katika Marathon Jumuia za Madola Glasgow 2014
Andrea Sambu (Left) |
Mwanariadha mkongwe nchini amefanikiwa kuingia ndani ya Qualification Standard ya
kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Jumuia ya Madola yanayotarajiwa
kufanyika mwakani mjini Glasgow Scotland.
Sambu alikimbia masaa 2:14:30 katika mashindano ya Donzhou Interanational Marathon nchini China December 21, 2013 kwa kumaliza akiwa nafasi ya tisa (9) na kufanikiwa kuingia ndani ya kumi bora.
Sambu alikimbia masaa 2:14:30 katika mashindano ya Donzhou Interanational Marathon nchini China December 21, 2013 kwa kumaliza akiwa nafasi ya tisa (9) na kufanikiwa kuingia ndani ya kumi bora.
Andrea Sambu
mwenye umri wa miaka 41 ndiye
mwanariadha pekee mtanzania aliyewahi kutwaa ubingwa wa dunia katika mbio za
nyika (World Cross Country
Championships) miaka 22 iliyopia (1991).
Bila shaka chama cha riadha RT kitamwandalia mazingira
mazuri Andrea Sambu kwani hadi sasa
yeye na Musanduki Mohamed pekee ndio
waliokimbia muda unaokubalika katika mashindano ya jumuia za madola katika nchi
nzima.
“Ninafurahi kwamba nimekuwa
katika ngazi ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 25 hadi sasa, nashindana na vijana
wadogo ambao wengine wana umri sawa ama chini ya umri wa watoto wangu” Sambu
alisema akiwa na furaha.
“Ningweza kushinda
mbio za juzi ila nililazimika kukaa Airpor ya KIA kwa siku nzima kutokana na
ndege ya Ethiopia kutua Arusha kwa dharura, hivyo nilisafiri kwa shida na
kufika China saa 10 alfajiri na kuunganisha mashindano saa moja asubuhi bila
kulala na uchovu wa flight ya zaidi ya masaa 15” Sambu aliendelea kuelezea.
Comments
Post a Comment