Wilbard Peter na Catherine Lange watwaa ubingwa Karatu Sports Festival
Catherine Lange @ Sokoine Marathon |
Leo mji mdogo wa Karatu uliopo jirani kabisa
na Ngorongoro Crater umeshuhudia mbio za kasi za umbali wa kilomita 10 zilizoshirikisha
wanariadha wa Tanzania.
Wilbard Peter wa Chuo cha Polisi Moshi (CCP) alishika
nafasi ya kwanza akifuatiwa na John Leonard wa Hakika Club na nafasi ya tatu
kuchukuliwa na Joseph Theophil wa Guang Club ya Mbulu.
Kwa upande wa wanawake mwanariadha mahiri
Catherine Lange wa timu ya Magereza Arusha alishinda, nafasi ya pili
ikidhibitiwa na Merry Naali wa Ambassador Club na nafasi ya tatu ikienda kwa
Angelina Tsere waWSSS.
Mtazamo: Kwa mtazamo wa haraka ni kwamba mbio
hizo zimefana kuliko mbio zilizokimbiwa hivi karibuni kwa kujali zaidi ushiriki
wa wanariadha wazalendo kwa kutozingatia ushiriki wa wanariadha kutoka nje ya
Tanzania.
Usumbufu unaojitokeza mara nyingi ni pale
ambapo MAWAKALA wa wakimbiaji wa nje ya nchi huwa wanafanya UHUNI wa
kuwadhulumu wakimbiaji wazalendo kwa kuwapendelea zaidi wakenya ili wao
MAWAKALA wajipatie ASILIMIA ndani ya Price Money ya wageni.
Sokoine Mini Marathon pia ilikuwa mbio iliyofana sana kwa kujali wanariadha wazalendo zaidi ili zawadi wanazopata ziweze kusitiri maendeleo yao hatimaye waweze kuwakilisha nchi yao vyema hapo baadaye.
Comments
Post a Comment