Baraza jipya la mawaziri: Safari hii rais Kikwete aamua kutumia subira yake mwenyewe, hamna presha, atatangaza wakati wowote
Dr. Mwakyembe & Dr. Magufuli |
Hata hivyo safari hii imekuwa tofauti kwani rais Kikwete ameamua kuumiliki uteuzi wake bila presha wala kuvuja kwa siri kabla ya siku yenyewe.
Watanzania hata hivyo wanayo imani kubwa kwamba rais atawateua watu wenye uzalendo na upendo kwa nchi yao, tofauti na mawaziri wengi walioshuhudiwa wakitumia nyadhifa zao vibaya kwa kutoa lugha korofi na zenye hadaa.
Taarifa za kuaminika zinabainisha kwamba "ugali tayari ila twasubiri ipoe kabla ya kuliwa". Muda wowote tutapata kujua nani yupo ama nani hayupo katika "Magic list of honorees"
Taarifa hiyo imeongeza kuwa "Dr. John Magufuli na Dr. Harison Mwakyembe ni kati ya mawaziri wasiokuwa na shaka wala homa katika kipindi hiki kigumu kama mawaziri wengine"
Wanajifahamu kwamba ni wachapa kazi wazuri na lazima watarudi barazani bila wasiwasi. Endelea kufuatilia habari hapa hapa!
Comments
Post a Comment