Georgina na Mallya waongoza vyema ‘Team Tanzania’ kuelekea ushindi wa jumla wa mashindano ya East African Junior Tennis Championships
Emmanuel Mallya |
Mashindano hayo yanayofanyika katika viwanja vya Gymkhana mjini Dar Es Salaam yalifunguliwa rasmi juzi na afisa mwandamizi wa wa International Tennis Federation ukanda wa Africa Mashariki ndugu Thiery Ntwari.
Hadi sasa timu machachari ya watoto mahiri wa kitanzania
inaongoza kwa uwingi wa waliovuka roundi ya kwanza.
Kwa upande wa vijana wanaume (under 16 yrs) Sadik Ibrahim amemshinda Mollazewdu Nehemia wa Ethiopia, Menard Frank akimbwaga Kigotho Olivier wa Kenya na Emannuel Mallya akifanikiwa kumshinda Hassane Maulida wa Comoros.

Wasichana under (16
yrs) Georgina Kaindoah alimshinda Zeru Maldhere wa Ethiopia na anatarajiwa kucheza tena leo na Nkata Judy wa Kenya.
Kwa mtiririko huu wavulana wote wa Tanzania wamefaniukiwa kuingia robo fainali huku msichana Georgina Kaindoah amefanikiwa kuingia nusu fainali.
Kwa mtiririko huu wavulana wote wa Tanzania wamefaniukiwa kuingia robo fainali huku msichana Georgina Kaindoah amefanikiwa kuingia nusu fainali.
Comments
Post a Comment