RAIS JAKAYA KIKWETE AMENISAIDIA KUWAPASHA VIONGOZI WA RT NA TOC;TAIFA ZIMA LINAWAOGOPA
DC asiyejali sheria za nchi |
'Niliiposti
habari hii 12/08/2013, JK akawapasha 19/01/2014'.
Hata hivyo Rais JK bado kuna siri hajaambiwa ya kwamba viongozi wa RT walivunja sheria NO. 12 za BMT zilizotungwa na Bunge 1967. Mtaka anadai kuwa "waziri Fenella ni shemeji yake na atamlinda, Nyambui pia ni ndugu yake wa ukoo" :
Wakati nchi za
ulimwengu zikiwakilishwa na wanariadha wake mahiri katika mashindano ya dunia
ya riadha mjini Moscow Urusi, Tanzania imevunja rekodi ya aina yake kwa
viongozi wa Chama Cha Riadha Tanzania kutangulia Moscow huku wakiwaacha
wanariadha nyuma.
Rais wa RT
(aliyechaguliwa kinyume na katiba) bila wasiwasi, aibu wala uzalendo amekwenda
Moscow wiki iliyopita huku walengwa wenyewe wa mashindano ya (World Athletic
Championships) ambao ni wanariadha wanaotegemewa kupeperusha bendera ya
Tanzania na kupigania medali wakibaki nyuma.
Cha ajabu zaidi ni
pale ambapo kiongozi huyo wa RT alipofuatana na kiongozi wa zamani wa chama
hicho kwa kile kinachodaiwa hana uzoefu katika mikutano ya Chama Cha Riadha duniani
(IAAF), kitu ambacho kinafanywa kuwa kisingizio cha viongozi hao kutangulia.
Kimsingi kiongozi
huyo wa zamani alikusudiwa kuwa kama kocha mwandamizi atakayefuatana na
wachezaji, ila sasa imekuwa sawa na rubani kuwaacha abiria nyuma. Sijawahi
kusikia kocha wa Taifa Stars akitangulia wiki moja kabla kwenye viwanja
vya matukio bila kuongozana na wachezaji wake, lakini kwa sababu RT ni mali ya
TOC hakuna cha kushangaza hadi hapo, watanzania waendelee kutafakari kwa kina
tabia hiyo mbaya inaendekezwa na nani, na kwa masilahi ya nani?.
Je inawezekana kwamba
rais huyo mtata wa RT anazungukwa na wajanja waliokwishaonja utamu wa fedha za
makampuni yaliyowahi kutudhamini?, nikimaanisha huenda kuna mpango unasukwa wa
kuitapeli makampuni kama ilivyokuwa PUMA na LINING?. Ili kiongozi
huyo wa RT mgeni asiyeelewa ‘umafya’ wa viongozi wa sasa na wa zamani wa
TOC wenye ushawishi mkubwa RT kutumika tu kama chambo (cheo) ili wajanja wale ‘sinia
kubwa’ wakati kiongozi mpya akifurahia posho (per day) huku taifa
likiendelea kupoteza sifa katika viwanja vya mchezo wa riadha, ‘masikini
taifa limetelekezwa na wahusika’. Ambao wangechunguza kiini cha matatizo ya
TOC na RT taifa lingekombolewa.
BMT na wizara
inayohusika na michezo inastahili kuwa na hisia ya maumivu pale Tanzania
inapojikuta nyuma kila wakati panapotokea mashindano ya kimataifa, swali muhimu
ni; Je wahusika wa TOC na RT wanalindwa na nani?, na ulinzi huo ni kwa masilahi
ya nani?, na ulinzi huo utaendelea hadi lini?.
Comments
Post a Comment