Kikwete awatia hofu watarajiwa wa uwaziri huku wengine wakifunga novena kumomba mungu wasipigwe chini

James Lembeli "The Man

Ikulu yageuka mbingu ya pili kwa kile kinachodaiwa sala zote lazima iombe huruma za mungu angalau rais awateue.
Hadi hii leo hii ni takriban mwezi mzima umepita tangu kutenguliwa kwa mawaziri wanne baada ya kuguswa moja kwa moja na kashfa ya Operation Tokomeza Ujangili.
Mawaziri waliolazimika kujiuzulu ni pamoja na Emmanuel Nchimbi - Mambo ya ndani, Shamsi Vuai Nahodha - Ulinzi, David Mathayo – Mifugo na Khamis Kagasheki – Maliasili na Utalii. 

Pigo lingine kwa baraza la mawaziri ni pale Tanzania ilipompoteza aliyekuwa waziri wa fedha Dr. William Mgimwa aliyefariki dunia masaa machache kabla ya mwaka 2014 kuanza.

“Rais Kikwete kipindi hiki ana kazi nzito ya kufanya; siyo kuteua mawaziri pekee! Kumbuka wabunge wa bunge maalum la katiba nao wapo katika process ya kuteuliwa” Chanzo cha kuaminika kilisema.

“Anaweza kuamua kuendelea na uteuzi wa wabunge wa katiba ndipo atangaze zote kwa pamoja” mtoa habari alisema hayo kwa kifupi. 

Ama kweli hatuna budi kumwachia mkuu wa nchi afanye kazi yake bila presha! Hata hivyo ‘is just the matter of time’

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga