Msiba chama cha Tennis: TTA yapata msiba mzito baada ya kocha wake mkongwe CHARLES KYANDO (TOLA) kufariki ghafla
Charles Kyando (Tola) Enzi za uhai wake |
Sekta ya michezo Tanzania imepata msiba mkubwa usiku wa
kuamkia leo kwa kufiwa na Charles Kyando
maarufu kwa jina la Tola, Kyando
alifariki ghafla baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Charles Kyando (Tola)
alizaliwa 1968 jijini Dar Es Salaam na wakati wa uhai wake aliwahi kucheza
mashindano mbalimbali ya mchezo wa tenisi na kufikia viwango vya kitaifa kati
ya miaka ya 1980 hadi 1990.
Baada ya kustaafu kama mchezaji bwana Kyando alikuwa kocha
wa mchezo wa tenisi na pia alikuwa mtaalam maarufu wa kusuka rakets za mchezo
huo.
Marehemu ameacha mjane na watoto wawili, pia marehemu
ameacha pengo kubwa na isiyozibika katika mchezo wa tenisi na katika chama cha
tenisi Tanzania (Tanzania Tennis
Association).
Kuhusu taratibu za mazishi na taarifa zozote kuhusiana na
msiba huu tafadhali endelea kusoma blogu hii ya Utaifa Kwanza.
Comments
Post a Comment