Mwandishi wa BBC Ann Waithera afariki: Shirika la habari la BBC limempoteza mwandishi wa habari Ann Waithera
Ann Waithera enzi za uhai wake |
Ann alikuwa anafanya kazi na BBC katika ofisi za Nairobi na amekuwa akiugua
Saratani ya Ubongo kwa karibu miaka miwili.
Ann aliwahi kuwa ripota wa BBC mjini Addis Ababa Ethiopia. Kabla ya kujiunga na BBC Ann alifanya kazi na shirika la habari la Nation
Media Group nchini Kenya na Citizen TV. Ann alikuwa na umri wa miaka 39.
Waandishi wenza wa Ann BBC wameelezea watakavyomkumbuka Ann katika enzi zake
alipokuwa anafanya kazi nao.
Razvan Scortea mmoja wa wakuu wa BBC amesema : "Nimeshtushwa sana na
kifo cha Ann. Alikuwa mtu mzuri , mwerevu mpenda watu na mwenye matumaini kwa
kila jambo. Mungu ambariki.''
Mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera ameelezea kuwa ni jambo la kuhuzunisha
sana kumpoteza Ann.
''Nimehuzinika sana. Anne alikuwa mwandishi mahiri . Kila nilipomtembelea
nilivutiwa sana na matumaini ya Ann kupona. Hata katika mkesha wa krismasi,
nilipozungumza na Ann alikuwa mcheshi sana. Nakumbuka Ann ndiye alikuwa
mwandishi wetu wa kwanza mwenye uwezo wa kuripoti katika lugha zaidi ya moja
mjini Addis Ababa Ethiopia,'' alisema Solomon
Mkuu wa idhaa ya kiswahili ya BBC Ali Saleh naye pia ameelezea kushtushwa
kwake na kifo cha Ann akimkumbuka kama mwandishi mahiri na mwenye kujitolea kwa
kazi zake.
'Nakumbuka kufanya naye kazi kabla ya yeye kwenda Addis Ababa, na kufanya
mipango ya kila alichotarajiwa kufanya. Matumaini mengi ila yamekatizwa mapema
mno.'' alisema Elizabeth Blunt aliyekuwa mwandishi wa BBC mjini Addis Ababa
kabla ya Ann kuchukua usukani kutoka kwake.
"Anne alikuwa mmoja wa waandishi mahiri wa BBC nchini Kenya . Kifo
kimetupokonya mmoja wa waandishi wenye talanta kuu Afrika Mashariki.'' Kauli ya
David Okwemba mhariri mkuu wa ofisi ya BBC Nairobi Kenya.
Mhariri mkuu wa idhaa ya Hausa mjini London Mansur Liman, ametuma rambi
rambi kwa familia ya Ann, akiwaombea utulivu wakati huu mgumu.
Comments
Post a Comment