SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA), limewapa beji waamuzi 10 wa Tanzania kwa mwaka 2014.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema orodha ya waamuzi hao wa kati na wasaidizi, wameipokea hivi karibuni kutoka makao makuu ya FIFA.

Wambura aliongeza kuwa hakuna waamuzi na wasaidizi walioongezeka katika orodha ya mwaka jana, hivyo idadi kubaki ile ile.

Aliwataja waamuzi wa kati waliopata beji hizo kuwa ni Ramadhan Ibada, Oden Mbaga, Israel Nkongo na Waziri Sheha.

Wambura aliwataja waamuzi wasaidizi kuwa ni Josephat Bulali, Ferdinand Chacha, Hamis Chang’walu, John Kanyenye, Ali Kinduli, Jesse Erasmo na Samuel Mpenzu.

Source: Tanzania Daima

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga