TANZIA: Mwandishi wa BBC Komla Dumor amefariki ghafla nyumbani kwake London kutokana na mshtuko wa moyo
Alikuwa na miaka 41 alipopata mauti yake.Komla Dumor
ameelezewa kuwa miongoni mwa waandishi shupavu barani Afrika.
Rais wa Ghana John Dramani Mahama amemtaja marehemu kama
zawadi ya Ghana ulimwenguni na kuongezea kuwa Ghana imempoteza mmoja wa wajumbe
wake.
Komla hivi karibuni alikuwa anaongoza kipindi cha Runinga
kinachozungumzia maswala ya Afrika baada ya kufanya kazi katika radio mmoja
nchini Ghana na vilevile radio ya BBC.
Mhariri wa habari za ulimwengu Andrew Whitehead amemtaja
kuwa mwadishi shupavu aliyekuwa na uhusiano mzuri na wasikilizaji.
Chanzo: BBC SWAHILI
Comments
Post a Comment