UTAIFA KWANZA: Mbio za kumbu kumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine zitafanyika Monduli mwezi Aprili 12, 2014
Mwaka huu Tanzania inaadhimisha miaka 30 tangu kifo cha aliyekuwa
waziri mkuu Hayati Edward Moringe
Sokoine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika dhifa hiyo
itakayofanyika kitaifa Monduli mahali alipozaliwa kiongozi huyo shupavu.
Madhumuni ya kuandaa mbio hizo ni kuthamini bidii, uzalendo na ujasiri aliotuonyesha wakati wa
uhai wake.
Watanzania wote wanaojali utu, haki, amani na Utaifa Kwanza
mnakaribishwa katika kumbu kumbu hiyo. ‘Tujikumbushe
baadhi ya nukuu zake akiwa waziri mkuu’
“Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi
wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na
Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda
tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo
vyao viovu” - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983.
“Katika nchi inayojali haki na
usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio
wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao
na kusahau maslahi ya walio wengi” - Edward Moringe Sokoine, 1 Februari 1977.
Comments
Post a Comment