BUNGE LA MICHEZO: "RIADHA HARD TALK 2014 MOSHI FEBRUARY 9 2014"
Domician Genandi |
Watanzania wameamua kuuvaa ukweli: Holili Youth Athletic Club iliyopo mkoani
Kilimanjaro inaandaa mdahalo utakaowashirikisha wanariadha wote, wadau na
viongozi wa chama cha riadha.
Mkurugenzi wa Holili Youth Athletic Club ndugu Domician Rwezaura Genandi
ameileza gidabuday.blogspot.com kwamba ameamua kufanya hivyo ili kutafuta kwa
pamoja jinsi ya kulipatia jawabu kiu ya medali ambayo Tanzania inayo kwa muda
mrefu.
“Ninaimani kwamba wote kwa pamoja tukiongea ukweli, kukosoana na kuelezana
ukweli tutapata jawabu mwisho wa mazungumzo ambayo yatratibiwa kwa uwazi na
ukweli” alisema mkuu huyo wa HYAC.
"Ikiwa Kweli tunapenda mchezo huu wa riadha; haijalishi wewe ni kiongozi,
mdau au mwanariadha basi mdahalo huu utaupenda maana sisi HYAC tumeamua
kugharimia ukumbi, chakula cha mchana wa siku hiyo na kuwapata waandishi na
vyombo vyao vya habari” aliendelea kusema Domician.
Utaifa Kwanza blog inawapongeza HYAC kwa wazo hili zuri ambalo RT
ingewachukua miaka Milioni kupata idea hiyo na kwamba ‘TUPO PAMOJA’ Siku hiyo
'Moshi itatoa Moshi mweupe kama alama ya ushindi wa kimawazo; solution ya kuleta
medali katika siku zijazo'.
Wanariadha wote mnaalikwa kusema kero zenu ili vyombo vya habari viweze
kupaiza sauti zenu wakuu wa nchi wapate kusikia na kufanyia kazi mawazo yetu ya
pamoja.
safi sana kaka Wilhelm endelea kutuabarisha na harakati za kufikisha riadha mbele daima.
ReplyDelete