Jamali Malinzi, wadau kumlipa Kim
Jamali Malinzi |
Malinzi, ambaye uongozi wake ulifanya kituo cha
kuteua wachezaji wa timu ya taifa badala ya kazi hiyo kufanywa na kocha,
pia jana aliongeza alitangaza kuwa fidia ya kuvunjwa kwa mkataba wa
Poulsen zitalipwa kwa ushirikiano baina ya TFF na wadao, ambao pia
hakuwataja.
Poulsen, ambaye analipwa mshahara na serikali
kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete, ana mkataba unaoisha Mei
mwakani na alipewa kazi hiyo baada ya kuonyesha mafanikio kwenye timu
za vijana.
Hivyo, kuvunjwa kwa mkataba huo kutalifanya
Shirikisho hilo limlipe Poulsen mishahara yake ya miezi sita kulingana
na mkataba wake. “Jukumu la kulipa gharama za kuvunja mkataba
zitabebwa na TFF na baadhi ya wadau wa soka watatusaidia nusu gharama,”
alisema Malinzi wakati alipoongea na waandishi wa habari jana kwenye
ofisi za Shirikisho.
Alipotakiwa awataje baadhi ya wadau hao, Malinzi alisema hata yeye ni mdau na kudai kuwa wako wengine wengi. Malinzi alithibitisha kuondolewa kwa kocha huyo na kwamba TFF inaendelea na mchakato wa kutafuta mrithi wake.
Tayari, TFF ipo kikaangoni ikilaumiwa na wadau
wake kwa uamuzi wa kubeba majukumu yasiyoihusu likiwamo la kuteua
wachezaji wa timu ya taifa ambayo itacheza mechi ya kirafiki na Namibia
wiki ijayo.
Kitendo cha TFF kuteua wachezaji wa timu ya taifa
kinaonekana kuwa kimepitwa na wakati kutokana na soka la kisasa kutaka
wataalaamu ndio wateue timu na kutetea uteuzi huo.
TFF pia inalaumiwa kwa uamuzi wake wa kusitisha
matumizi ya tiketi za kielektroniki bila ya kufanya utafiti yakinifu wa
matatizo ya mfumo huo.
TFF pia inalaumiwa kwa uamuzi wake wa kuchezesha
mechi za kombaini ya mikoa kwa lengo la kuibua vipaji kwa ajili ya timu
ya taifa itakayokuwa ikisaka tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya
Afrika za mwaka 2015.
Kuhusu mrithi wa Poulsen, Malinzi alisema wapo
katika hatua za mwisho za kumpata kocha ambaye alisema huenda atatoka
Uholanzi au Ujerumani.
CHANZO: Mwananchi
CHANZO: Mwananchi
Comments
Post a Comment