Rais Jakaya Kikwete mgeni rasmi Sokoine Mini Marathon Monduli
Watanzania wote wanakaribishwa katika kumbu kumbu ya miaka 30 tangu kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine.
Katika tamasha la mwaka huu kutakuwa na mbio za Half Marathon (21km) ambazo zitakimbiwa na wanariadha wazoefu (Elite Athletes). Pia kilomita 2 kwa ushiriki wa wanafunzi na waheshimiwa wetu wa serikali, wanajeshi na vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama.
Mwaka jana mbio hizo zilifana kwa kuruhusu jamii kushiriki
mbio bila kujali mavazi yao ya kitamaduni, wanafunzi pia walishiriki na
kuonyesha vipaji vyenye sifa ya kuiletea Tanzania medali kwa miaka ijayo.
Pia kutakuwa na mashindano ya kurusha mkuki na kuruka chini
kwa wanaume pekee, ngoma za asili pia zitachezwa kwa ajili ya burudani nk. Hii ni fursa ya kutangaza utalii pia.
Comments
Post a Comment