Rogart John, Phaustin Baha na Gidabuday wakiwaza namna ya kuhamasisha riadha


Rogarth, Faustin & Gidabuday/Photo by Gadiola
Siku ya kwanza kuwaza mbinu za kupeleka wazo la Sokoine Mini Marathon kwa wahusika tulikuwa watatu na ilikuwa kazi sana kutokana na upinzani kutoka kwa wanaojiita ‘Viongozi wa RT/TOC’


Kila mtanzania anayo jukumu la kubuni mbinu mbadala kusaka vipaji, kukuza vipaji na kuhamasisha taifa kuwa mstari wa mbele kuchangia gharama za timu zetu za vijana hatimaye kufuzu timu za taifa.


Lakini kwa bahati mbaya Ubinafsi, Wivu na Ukabila umetawala katika chama cha riadha na kamati ya Olimpiki. Kwa mawazo yao “Bila Filbert Bayi na Suleiman Nyambui watanzania hawawezi lolote”. Wamefanikiwa kuwaaminisha wengi kwa kuwapotosha ili wao watukuzwe.


Hadi leo ni wazi kwamba Sheria # 12 za BMT zilizotungwa na Bunge 1967 zilivunjwa makusudi ili kuwazuia watu wawili tu wasiingie katika uongozi wa RT! Je Bayi, Nyambui na Mtaka wana nguvu kumshinda Jakaya Kikwete anayesisitiza sheria kufuatwa?.


Bila shaka tutakuwa na JK siku zijazo na tutamweleza siri asiyeijua na kwanini waliamua kuvunja sheria za nchi?. Wangekuwa na uwezo naamini hata ‘JESHI LA UASI WANGEUNDA’.


April 11, 2013 Filbert Bayi alijichimbia hoteli moja maarufu Arusha na kuwaita wanariadha na waamuzi walioandaliwa kwenda kufanikisha mbio za Sokoine; aliwasihi wasiende kushiriki ili mbio hizo zikwame! Nashukuru wanariadha na waamuzi walimkubalia lakini asubuhi na mapema wakaja Monduli sababu wamejua kwamba mzee huyo hana uzalendo tena!


Ni wazi sasa kwamba umaarufu wa Filbert Bayi unashuka kutokana na ukweli kuhusu utu wake kuendelea kujitokeza! Hata shughuli za kiserikali anataka kuziharibu?


Watanzania sasa wameamua kwamba haogopwi mtu! Hata kama wanatutishia kutupeleka Msitu wa Mwabepande! 

April 12 watanzania tukutane Monduli tumkumbuke Sokoine aliyechukia Ufisadi na Ubinafsi ambao unaendekezwa na TOC pamoja na RT.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga